TWAA

Moyo na nafsi ya mwanadamu imeumbwa katika maumbile na tabia ya kufuata au kutofuata inayoelekezwa na kuamrishwa kutenda au kutotenda.

Nafsi inapojijengea utamaduni wa kufuata na kutekeleza iliyoamrishwa na kujiepusha na kuyaacha iliyokatazwa, hiyo ndiyo twaa (utii) na mtu mwenye nafsi yenye sifa hizo huitwa mtiifu.

Imempasa na kumlazimu mwanadamu kumtii Mola Muumba wake, kumtii mtume wa Mwenye Mungu na watawala wanaotawala kwa kufuata muongozo wa Mwenyezi Mungu, haya ni kwa mujibu wa kauli ya Mola isemayo:-

“ENYI MLIOAMINI! MTIINI MWENYEZI MUNGU NA MTIINI MTUME NA WENYE MAMLAKA JUU YENU, WALIO KATIKA NYIE(Waislamu wenzenu)”(4:59)

Hii ni twaa ya kwanza kabisa, twaa ya pili ielekezwe kwa wazazi. Wazazi wako ndio sababu ya kuwepo kwa leo katika maisha haya,

Na wamepata taabu, mashaka na shida chungu nzima katika kukuzaa, kukulea na kukuelimisha mpaka ukawa mtu mzimajunayeweza kuyasimamia mambo yako mwenyewe. Kwa kuyazingatia yote haya Mwenyezi Mungu anatuamrisha:

“MOLA WAKO AMEHUKUMU KUWA MSIMUABUDU YOYOTE ILA YEYE TU NA (ameagiza) KUWAFANYIA WEMA(mkubwa) WAZAZI KAMA MMOJA WAOAKIFIKIA UZEE, (naye yuko) PAMOJA NAWE, AU WOTE WAWILI, BASI USIWAAMBIE HATA AH! WALA USIWAKEMEE NA USEME NAO KWA MSEMO WA HISHIMA(kubwa). (17:23))

Twaa ya tatu ni kuwatii wanawazuoni na walimu. Wakati ambapo mzazi humlea mwanawe kimwili kwa kumpa chakula, mavazi na mahala pa kulala mwalimu humlea mtoto kiroho na kiakili, vitu viwili hivi roho na akili ndivyo humfanya mtu kuwa mwanadamu kamili aliyetofautiana na viumbe hai vingine.

Mwalimu ndiye sababu ya mtoto kumjua mola wake, kuijua daraja ya wazazi wake, kuijua dini yake na ulimwengu wake.

Kwa sababu hizi na nyingine tusizozitaja imempasa mtoto/mwanafunzi kumtii, kumuheshimu na kumpenda mwalimu wake na kutokasirika anapomtia adabu.

 

TWAA

Moyo na nafsi ya mwanadamu imeumbwa katika maumbile na tabia ya kufuata au kutofuata inayoelekezwa na kuamrishwa kutenda au kutotenda.

Nafsi inapojijengea utamaduni wa kufuata na kutekeleza iliyoamrishwa na kujiepusha na kuyaacha iliyokatazwa, hiyo ndiyo twaa (utii) na mtu mwenye nafsi yenye sifa hizo huitwa mtiifu.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *