NAMNA YA KUTAYAMAMU

Kwa kuwa tayari tumeshathibitisha kwamba tayamamu ni sheria katika uislamu, sheria hii haikuachwa ielee angani na kumpa fursa kila mtu aitekeleze kwa mujibu wa matakwa na matashi yake.

Sheria hii imewekewa utaratibu maalumu wa kuitekeleza na mwenyewe Mwenyezi Mungu na kubainisha na Bwana Mutume kiutendaji.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia ndani ya Qur-ani:

“………. BASI KUSUDIENI (tayamamuni) UDONGO (mchanga) ULIO SAFI (twahara) NA KUUPAKA NYUSO ZENU NA MIKONO YENU….…..” (5:6).

Haya ni maelekezo na maelezo ya jumla kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia tutayamamu kwa kutumia mchanga, tuzipakaze nyuso na mikono yetu.

Swali linajitokeza tupakaze vipi, namna ya upakaji inakuwa je ?

Hapa sasa ndipo inapoonekana nafasi na umuhimu wa Bwana Mtume na kwamba bila yeye dini hii haieleweki na wala haitekelezeki.

Yeye ndiye aliyetoa maelezo na kuonyesha namna ya kutayamamu mbele ya maswahaba ili kuitekeleza kiutendaji aya hiyo na kuufundisha uma jinsi ya kuitekeleza sheria hii ya tayamamu.

 Sasa basi ili tayamamu ya mtu ikubalike kisheria ikiwa ni pamoja na ibada atakayoifanaya kwa tayamamu hiyo ni lazima ahakikishe kuwa anatayamamu kwa mujibu wa utendaji na maelekezo ya Bwana Mtume.

Ifuatayo ndiyo namna ya kutayamamu kama alivyofundisha Bwana Mtume:-

Kwanza kabisa andaa mafungu/marundo mawili ya mchanga ulio twahara.

Halafu elekea Qibla, sema; BISMILLAAH, piga mikono yako juu ya fungu moja la mchanga huku ukisema moyoni mwako NAWAYTUS – TIBAAHATI FARDHWIS – SWALAA

Kung’uta mchanga kidogo na upakaze uso wako kwa mikono yote miwili vumbi lililobakia katika vitanga hivyo kama unavyouosha uso katika udhu.

Halafu piga tena kwa vitanga vyako katika lile fungu la pili la mchanga, kung’uta mikono yako kidogo.

Kisha upakaze mkono wa kulia kwa mkono wa kushoto na upakaze ule wa kushoto kwa mkono wa kulia.

Zingatia kupakaza vumbi ni mara moja moja tu na sio mara tatu kama ilivyo katika kutawadha.

NAMNA YA KUTAYAMAMU

Kwa kuwa tayari tumeshathibitisha kwamba tayamamu ni sheria katika uislamu, sheria hii haikuachwa ielee angani na kumpa fursa kila mtu aitekeleze kwa mujibu wa matakwa na matashi yake.

Sheria hii imewekewa utaratibu maalumu wa kuitekeleza na mwenyewe Mwenyezi Mungu na kubainisha na Bwana Mutume kiutendaji.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *