HURUMA

Huruma ni pambo analotakiwa kujipamba nalo muislamu kwa sababu hii ni sifa inayomsaidia kwa kiasi kikubwa sana kuyatekeleza baadhi ya mafundisho ya dini yake.

Huruma tunayoikusudia kuizungumzia hapa ni ile sifa ya kimaumbile iliyomo ndani ya mwanadamu. Sifa hii ndio chachu inayoamsha hisia za hurma ndani ya mtu na kumsukuma kuwahurumia wanadamu wenziwe na viumbe wenngine pia.

Kila mwanadamu huzaliwa akiwa na sifa hii ya kimaumbile. Huruma hii ya kuzaliwa/ya kimaumbile hueza kuongezeka au kupungua. Mazingira, wazazi na malezi {mafundisho} ya kidini yana mchango mkubwa sana katika kuikuza huruma ya mtu.

Mtoto akizaliwa na wazazi wake wakamuonyesha moyo wa upendo na huruma, akakua katika mazingira yaliyotawaliwa na huruma na kufundishwa mafunzo ya dini, huyu bila ya shaka atakuwa anatawaliwa zaidi na hurma katika maisha yake ya kibinafsi na yale ya kijamii.

Huruma ikishaota mizizi na kukita ndani ya mtu hairidhii kuendelea kubakia ndani bali hujitokeza nje ya mtu kupita kauli na matendo yake mbalimbali, na hili ndilo tuhitalo tunda la huruma. Matunda ya huruma ni pamoja na:-

Mwenye nguvu kumnusuru na kumsaidia nduguye mnyonge.

Huruma ikiutawala moyo wa mtu, haitompa fursa mwenye nguvu kumuonea au kukubali mnyonge aonewe na kunyimwa haki mbele yake nae akiangalia tu na kusema haimuhusu. Bali huruma ya kweli itamsukuma kuchukua hatua za makusudi kadri ya uwezo wake kumnusuru na kuhakikisha kuwa mnyonge haonewi wala kunyimwa haki anayoistahili eti tu kwa sababu ya unyonge wake. Kwa kufanya hivyo, huruma itakuwa imemsaidia huyu mwenye nguvu kuitekeleza kauli ya Mola wake:

“— NA SAIDIANENI KATIKA WEMA NA TAQ-WA, WALA MSISAIDIANE KATIKA DHAMBI NA UADUI —“ [5:2]

Mwenye huruma ya kweli atamsaidia mdhulumiwa.

Imani ya Kiislamu kupitia idara huruma, haimpi muislamu nafasi ya kudhulumu au kukubali kudhulumiwa seuze kuridhia mtu adhulumiwe.

Huruma ya kimaumbile iliyostawishwa na mafunzo ya Uislamu, inampa Muislamu ujasiri wa kumkemea dhalimu na kumwambia wewe ni dhalimu, acha udhalimu kwani Allah hapendi dhuluma kama asivyowapenda Madhalimu.

Ikiwa hakunasihika, basi Uislamu unamtwisha muumini jukumu la kuiondosha dhuluma. Muislamu anatakiwa aseme

“AKASEMA: “AMA ANYEDHULUMU BASI TUTAMUADHIBU, KISHA ATARUDISHWA KWA MOLA WAKE NAYE ATAMUADHIBU ADHABU MBAYA KABISA.”] (18:87)

Waislamu wanaambiwa: “— MSIDHULUMU WALA MSIDHULUMIWE.” [2:279]

Hebu usikize na huu wito wa Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie:

“Mnusuru nduguyo akiwa ni dhalimu au mdhulumiwa –.”

Mnusuru dhalimu kwa kumkemea aache kudhulumu na mdhulumiwa asidhulumiwe, Je, kama hakuna chembe ya huruma moyoni, mtu atashughulika na kumsaidia mdhulumiwa?

Mwenye huruma atakuwa tayari kumpokea na kumuhifadhi mkimbizi wa haki.

Tunasema mkimbizi wa haki, kwa sababu yawezekana kabisa mtu akawa ni dhalimu huko aliko, siku moja akashindwa na nguvu za wadhulumiwa.

Hawa wakataka kumkamata ili aadhibiwe kwa mujibu wa sheria, lakini bahati ikawa upande wake, akaponyoka na kuwa mkimbizi mahala fulani.

Huyu ni mkimbizi haramu, hana nafasi ya kuonewa huruma hata chembe, arudishwe kwao akalipie dhuluma aliyoifanya.

Muhajirina {Maswababa waliohamia madinah} ni mfano mzuri tunaoweza kuupiga wa wakimbizi wa haki na Ansari {Maswabaha wenyeji wa Madinah} ni kigezo chema kinachoonysha ni jinsi gani huruma iliyotawaliwa na malezi bora ya kidini inavyofanya kazi. Ansari wanatuonyesha namna njema ya kuwapokea wakimbizi, tusome

“— NA WAKAWAPENDA HAO WALIOHAMIA KWAO {Wakimbizi wa Imani}, WALA HAWAPATI, HAWAONI DHIKI NYOYONI MWAO KWA HAYO WALIYPEWA {hao Muhajiri – wakimbizi} NA WANAWAPENDELEA KULIKO NAFSI ZAO INGAWA WENYEWE WANA HALI NDOGO —.” [59:9]

Huruma ya mwenye huruma pia itajitokeza kupitia namna ya uzungumzaji wake na watu na kuchanganyika nao kimaisha.

Huruma itamsukuma kuongea na watu katika mazingira ya kirafiki na upole huku akijali hisia na mawazo yao Muislamu atafanya hivyo kwa kuitekeleza amri ya Mola wake:

“— NA SEMENI NA WATU KWA WEMA —.” [2:83]

Naam, ni muhali kusema na watu kwa wema ikiwa huna huruma, lazima kuwepo na kichocheo.

Mwenye huruma ni muadilifu.

Huruma ndio chachu inayomfanya mtu kuwa muadilifu, jambo ambalo ni miongoni mwa misingi iliyojengwa juu yake uislamu

“KWA HAKIKA ALLAH ANAAMRISHA UADILIFU NA KUFANYA HISANI –.” [16:90]

Huruma ya mtu pia huonekana kupitia namna anavyowashughulikia mayatima.

Mayatima ni sehemu isiyotengkea ya jamii inayohitaji huduma na malezi ya pekee. Dhima ya kuilea jamii hii ya mayatima hi jukumu la kila mmoja wetu.

Kuwajali na kushughulikia mayatima ni dalili na ishara tosha inayoonyesha sura ya jamii iliyojengwa katika misingi ya huruma na upendo wa dhati.

Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa ukitaka kujua kama jamii Fulani ni huruma {makatili} itizame kupitia mayatima wake.

Ikiwa inawajli mayatima, basi fahamu kuwa hiyo ni jamii ya watu wenye huruma na kama haiwajali, basi elewa kwamba hiyo ni jamii ya watu makatili wsio na huruma.

Kuhusiaa na suala la mayatima Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia ndani ya Qur-ani tukfu:

 “— NA MUWFANYIE WEMA WAZAZI NA JAMAA NA MAYATIMA NA MASIKINI —.” [2:83] Tusome tena: [— NA WANAKUULIZA JUU YA MAYATIMA SEMA: “ KUWATENDEA MEMA NDIVYO VIZURI. NA KAMA MKICHANGANYIKA NAO (Ndivyo vyema vile vile) KWANI NI NDUGU ZENU —) (2:220)

 haya ni baadhi tu  ya matunda yanayozalishwa na tabia ya huruma kama mmea au mti na pia ndio sura ya huruma aliyonayo mtu inayoonekana machoni mwa jamii.

Tunaweza kuigawanya sifa/tabia hii ya huruma katika matapo/makundi manne yafuatayo:-

i/.         Huruma binafsi: hii ni huruma inayomuhusisha mtu na nafsi yake tu.

 Aina hii ya huruma mwenyewe kwa kuhakikisha kuwa hajitii matatani kwa namna ye yote ile iwayo.

Humchochea kutekeleza maamrisho ya Mola wke na kujiepusha na makatazo yake ili asalimike na adhabu ya Mola wake leo duniani na kesho kule akhera.

ii/.        Huruma familia. Hii ni aina ya huruma inayomuhusisha mtu na familia yake.

Huruma hii humuamassha mtu kuionea huruma familia yake kwa kuitendea yale ambayo yatailetea furaha, na matumaini sambamba na maisha mazuri na mema ya duniani na kule akhera.

Pia hufanya juhudi za makusudi kuiepusha familia yake na yale yote yatakayokuwa ni sababu ya huzuni, majuto na maisha mabaya ya ulimwengu huu a sasa na ule ujao. Atayafanya yote haya kwa kuamrika na amri ya muumba wake:

“ ENYI MLIOAMINI JIOKOENI NAFSI ZENU NA WATU ENU NA MOTO AMBAO KUNI ZAKE NI WATU NA MAWE —“ [66:6] Tuzidi kusoma kwa mazingatio: “NA WAAMRISHE WATU WAKO KUSWALI, NA UENDELEE MWENYEWE KWA HAYO —.” [20:132]

iii/.       Huruma jamii: hii ni huruma inayomuhusisha mtu na jamii ya wanadamu wenziwe bila kuwasahau viumbe wengine kama vile wanyama, ndege na kadhalika.

Huruma hii itamfanya mtu ashughulike, na kuyajali maslahi ya jamii yake zaidi kuliko maslahi yake binafsi.

Atajitoa muhanga kuitumikia jamii yake katika yale yote ambayo mna ndani yake radhi ya Mola wake.

Atayafanya yote haya kwa kuwa daima ngoma ya masikio yake inagongwa na kauli ya Mtume wake Rehema na Amani zimshukie: Si katika sisi asiyeshughulika/asiyejali masuala ya waislamu (jamii) wenziwe.

iv/.       Huruma huduma: Aina hii ya huruma humuhusisha mtu na mtumishi wake wa nyumbani au muajiriwa wake ofisini, shambani, kiwandani na mahala popote pale panapotoa ajira.

Huruma hii itambana muajiri kumuonea huruma muajiriwa wake kwa:-

Kumpa mshahara unaokidhi mahitaji yake.

Kumjali katika hali ya ugonjwa au msiba.

Kushughulikia mafao yake ya uzeeni.

Kumthamini utu wake

Kutomkalisha kufanya kazi asiyoiweza, au kumfanyisha kazi kwa muda mwingi bila ya mapumziko.

Kutotumia lugha ya matusi na ukali katika maelekezo yoyote yahusianayo na kazi, kwani yote haya humuathiri kisaikolojia.

Kama ni mtumishi wa nyumbani amjengee mazingira ya kujihisi kuwa ni mmoja wa familia yake. Asimbague katika kula, ikawa yeyue ana chakula maalum na mtumishi anapewa chakula asichoweza kukila yeye.

Hivi ndivyo tunavyoweza kuigawa sifa/tabia hii ya huruma ambayo ni sehemu ya maumbile ya mwanadamu.

Huruma ndio iliyokuwa siri kuu ya mafanikio aliyoyapata Mtume wa Allha Rehema na Amani zimshukie.

 Aliitumia huruma kama chombo ha kumkusanyia na kumletea karibu jamii yake na hivyo kuifanya kazi yake kuwa rahisi.

Mwenyezi Mungu mtukufu aamkumbusha juu ya hili

 “BASI KWA SABABU YA REHEMA ITOKAYO KWA ALLAH UMEKUWA LAINI KWAO (Ewe Muhammad) NA KAMA UNGEKUWA MKALI NA MWENYE MOYO MGUMU BILA SHAKA WANGALIKUKIMBIA —.” [3:159]

 

HURUMA

Huruma ni pambo analotakiwa kujipamba nalo muislamu kwa sababu hii ni sifa inayomsaidia kwa kiasi kikubwa sana kuyatekeleza baadhi ya mafundisho ya dini yake.

Huruma tunayoikusudia kuizungumzia hapa ni ile sifa ya kimaumbile iliyomo ndani ya mwanadamu. Sifa hii ndio chachu inayoamsha hisia za hurma ndani ya mtu na kumsukuma kuwahurumia wanadamu wenziwe na viumbe wengine pia.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *