KUWA NA HURUMA

Muislamu unausiwa na kuhimizwa kujipamba na tabia ya huruma kamili kwa viumbe wote wa Allah; wanadamu wenzio na wasio wanadamu. 

Ishi na wanadamu wenzio na changanyika nao kimaisha kwa kuwaonyesha upole na huruma.  Uwe mpole na mwenye huruma hata kwa wale walio maadui zako na wanaokufanyia hasadi katika neema ulizopewa na Mola wako. 

Ni wajibu wako kutambua kwamba mwanadamu ikiwa ni pamoja na wewe mwenyewe ni kiumbe dhaifu:

“…MWANADAMU AMEUMBWA DHAIFU (hana nguvu kubwa kabisa za kiwiliwili wala nguvu kubwa  za kupigana na moyo na shetani).”  (4:28). 

Ukiri udhaifu huu wa mwanadamu ambao ni sehemu ya maumbile yake na umuhurumie.

Umuhurumie na umchukulie upole hata adui yako, kwani kwa yakini Allah Mola Mwenye huruma huwaonea huruma waja wake wenye kuwaonea huruma wanadamu wenzao.

 Hivi ndivyo unavyoambiwa na Mtume wako–Rehema na Amani zimshukie:

“Wenye huruma watahurumiwa na Mwingi wa rehema (Allah), wahurumieni walioko ardhini (viumbe wenzenu) atakuoneeni huruma aliyeko  mbinguni (Mola muumba wenu)”. Ahmad, Abuu Daawaud, Tirmidhiy & Al-Haakim

Ni bora na ni kheri kwako ukamuhurumia mwanadamu mwenzio kwa udhaifu wake, kwani kumbuka kwamba asiyehurumia ahurumiwi.

Hebu jiulize, je wewe hutaki huruma ya Allah Mola Mwenye huruma? Kama unaitaka, basi itafute huruma hiyo kwa kuwahurumia viumbe wenzio kila unapowapata udhaifu wa kibinadamu.

Huruma yako hii isikomelee tu kwa wanadamu wenzio bali iwaenee hata wanyama ambao Allah amewaumba kwa ajili ya manufaa yako. 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah–Allah amuwiye radhi–kwamba Mtume wa Allah-Rehma na Amani zimshukie amesema:

“Wakati ambapo mtu mmoja akienda njiani, kikamshika kiu kikali kabisa akashuka kisimani akanywa maji humo, kisha akatoka (kuendelea na safari yake). Tahamaki huyo mbele yake ni mbwa anahema na kula mchanga kutokana na ukali wa kiu. Akajisemea: Bila ya shaka kimempata (mbwa) huyu kiu kama kilichonipata mimi (hivi punde tu).  Akakijaza maji kiatu chake kisha akakiuma kwa mdomo wake, akapanda (kutoka kisimani mle). Akaja akamnywesha maji mbwa yule, Allah akakishukuru kitendo chake kile cha huruma, akamsamehe dhambi zake kwa sababu hiyo. (Maswahaba) wakauliza: Ewe Mtume wa Allah, hivi sisi tuna ujira kwa (kuwatendea huruma hata) wanyama! Mtume akawajibu: “Katika kila ini bichi (kilicho hai) kuna ujira.”  Bukhaariy

Hebu ndugu muislamu na tuienzi kauli hii ya Mtume wetu–Rehema na Amani zimshukie-kwa kuwaonea huruma wanyama:

“Mwenye kukihurumia walau kichinjwa cha ndege, Allah atamuonea huruma siku ya kiyama.” Bukhaariy, Twabaraaniy & Dhwiyaa

Elewa kumuhurumia kiumbe dhaifu mithili ya ndege unayetaka kumchinja kwa ajili ya kitoweo chako si kuacha kumchinja.  Bali ni kutokumtesa au kumchinja kikatili.

 

KUWA NA HURUMA

Muislamu unausiwa na kuhimizwa kujipamba na tabia ya huruma kamili kwa viumbe wote wa Allah; wanadamu wenzio na wasio wanadamu. 

Ishi na wanadamu wenzio na changanyika nao kimaisha kwa kuwaonyesha upole na huruma.  Uwe mpole na mwenye huruma hata kwa wale walio maadui zako na wanaokufanyia hasadi katika neema ulizopewa na Mola wako. 

Ni wajibu wako kutambua kwamba mwanadamu ikiwa ni pamoja na wewe mwenyewe ni kiumbe dhaifu:

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *