MAMBO YALIYO HALALI KUFANYA NDANI YA SWALA

Mswaliji anaruhusiwa kisheria kufanya baadhi ya mambo akiwa ndani ya swala, kwa sharti kwamba kuwe na dharura ya kufanya hivyo.

Anaruhusiwa kuyafanya mambo hayo katika hali hiyo ya dharura bila ya swala yake kubatilika. Mambo hayo ni kama yafuatavyo:-

  • Ni halali kufanya kitendo kichache/chepesi. Kitendo hiki ni kama vile mtu kufunga shuka/msuli wake uliolegea ambao kama hakuufunga (hakuukaza) utamuanguka.

    Na kumuacha utupu na hivyo kupelekea kubatilika kwa swala yake.

  • Kujikohoza wakati wa haja. Ni jambo lililoruhusiwa mtu kujikohoza ikiwa kapaliwa na kitu au kohozi limemkaa kohoni.
  • Kumuweka sawa mtu katika safu. Ni rukhsa kumvutia mbele au nyuma mtu aliye nje ya safu ili akae sawia katika safu.

Kadhalika ni rukhsa Imamu kumzungushia maamuma kuliani kwake ikiwa atakuja na kusimama kushotoni   kwake, wakati ambapo wako wawili tu yeye na imamu.

Hivi ndivyo mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alivyofanya kwa Ibn Abbas-Allah amuwiye radhi-aliposimama kuswali pembeni yake usiku. Haya ni kwa mujibu wa riwaya ya imamu Bukhaariy.

  • Kupiga mwayo na kufunika kinywa kwa kiganja cha mkono. Mswaliji anaruhusiwa kufunika kinywa chake kwa kiganja cha mkono wake atakapopiga mwayo ndani ya swala.
  • Kumfungua/kumzindua Imamu wake atakaposahau au kukwama katika kisomo. Ni halali kwa maamuma kumfungua Imamu wake anapokwama katika kisomo cha Qur-ani.

Kama ambavyo pia ni halali kumzindua atakapoacha au kuzidisha nguzo kwa kutamka: (Sub-haanallah). Rukhsa hii inatokana na kauli yake Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie: “Atakayepatwa na jambo ndani ya swala yake na aeme: Sub-haanallah”. Bukhaariy & Muslim

  • Kumzuia mtu apitaye mbele yake. Mswaliji anaruhusiwa kumzuia kidogo na hata kwa nguvu mtu apitaye mbele yake.

Uhalali huu anaupata kutokana na kauli ya Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie: “Atakaposwali mmjoa wenu kuelekea kitu kinachomsitiri na watu, atakapotaka mtu kupita mbele basi na amzuie. Akikataa basi na amzuie kwa nguvu, kwani huyo ni shetani”. Bukhaariy & Muslim

  • Kumuua nge au nyoka. Ikiwa mswaliji atatokewa na nge au nyoka akiwa ndani ya swala yake, sheria inamruhusu kumuua nge au nyoka huyo.

Lakini anachotakiwa kufanya ni kitendo cha kuua tu na sio kutamka maneno yaliyo nje ya swala. Kwani kufanya hivyo kutapelekea kubatilika kwa swala.

Matendo yote atakayoyatenda mpaka kumuua nge au nyoka huyo yatasameheka na ataendelea na swala yake bila ya kubatilika. Rukhsa hii ni natija ya kauli yake Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie: “Viuweni vyeusi viwili ndani ya swala; nyoka na nge”. Tirmidhiy

  • Kujikuna, mswaliji anaruhusiwa kujikuna panapomuwasha katika mwili wake. Kwa sababu kujikuna ni katika matendo machache/mepesi yenye kasameheka ndani ya swala.
  •   Kumuashiria kwa mkono mtu aliyemtolea salamu, hili linatokana na kitendo cha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie. Kama ilivyo katika riwaya ya Imamu Tirmidhiy.

Kauli jumla ni halali kufanya kila tendo ambalo halipingani/halikinzani na adabu, suna au unyenyekevu wa swala. Kama vile mtu kutoa machozi anaposoma aya inayotoa onyo kali au inayofanya adhabu.

 

 

 

 

MAMBO YALIYO HALALI KUFANYA NDANI YA SWALA

Mswaliji anaruhusiwa kisheria kufanya baadhi ya mambo akiwa ndani ya swala, kwa sharti kwamba kuwe na dharura ya kufanya hivyo.

Anaruhusiwa kuyafanya mambo hayo katika hali hiyo ya dharura bila ya swala yake kubatilika. Mambo hayo ni kama yafuatavyo:-

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *