SHAHADA MBILI NI NINI?

Shahada mbili ni mkusanyiko wa matamko mawili ya ahadi anayoichukua kiumbe (mwanadamu) mbele ya Muumba wake na viumbe wenzake.

Ambapo mtamkaji hula kiapo cha utii kwa Allah Mola Mwenyezi na Mtume wake katika maisha yake yote kwa kufuata maamrisho na makatazo yake.

1. SHAHADA YA KWANZA – TAMKO LA UTII KWA ALLAH:

            Ni mtu kutamka kwa moyo na ulimi:-

        “ASH – HADU AN LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU”

Maana : “Ninakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kwamba  hapana afaaye kuabudiwa kwa haki ila  Allah (Mola asiye na mshirika wala mwana)”

     2.   SHAHADA YA PILI: TAMKO LA UTII KWA MTUME WA ALLAH.

            Ni mtu kutamka kwa moyo na ulimi:-

“WA ASH-HADU ANNA MUHAMMADAN ABDUHU WA RASUULUHU”

Maana: “Na ninakiri kwa moyo natamka kwa ulimi kwamba Muhammad ni mja na mjumbe wa Allah (kama alivyo Isa, Musa, Ibrahimu)

Matamko mawili haya ya ahadi ndio tiketi ya kuingilia katika Uislamu baada ya mtu kujitoa mwenyewe.

Mtu akiyatamka maneno haya tu tayari anakuwa muislamu tena na papo hapo anawajibika kuishi chini ya kivuli na mipaka ya shahada mbili hizo.

Kwani kuishi kwa mujibu wa shahada mbili ndiko kutampa sifa ya kuwa muumini mbele ya Alah Mola Muumba wake na mbele ya viumbe (waumini) wenzake.

Leave a Reply

Your email address will not be published.