SIKIO SIKIVU

Miongoni mwa watu waliokuwa mbele ya mpishi wa fitna hii iliyokurubia kuwagawa waislamu kwa misingi ya Umakkah na Umadinah.

Alikuwa ni kijana mdogo ambaye bado hajafikilia baleghe; Zayd Ibn Arqam, huyu akaichukua khabari ile ya maneno ya Abdullah Ibn Ubayyi na kumfikishia Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie.

 Akampasha khabari hiyo akiwa pamoja na kundi la watu kadhaa katika Muhajirina na Answari. Pale pale uso wa Mtume wa Allah ukabadilika na kusema:

 “Ewe kijana huenda wewe una chuki nae?” Akajibu:

“Wallah, hapana kwa yakini nimemsikia”. Mtume akazidi kumuhoji:

“Huenda masikio yako hayakusikia vizuri”, akajibu:

“Hapana, ewe Mtume wa Allah!” Akamuuliza tena ili kupata ithibati:

“Huenda umechanganya maneno kutokana na kutatizwa”. Akajibu:

“Wallah hapana, kwa yakini nimemsikia akisema ewe Mtume wa Allah!”

Basi yakatangaa na kuenea kambi nzima maneno aliyoyasema Ibn Ubayyi mpaka ikafikia watu hawana kingine cha kuzungumzia ila maneno hayo. Sayyidina Umar Ibn Al-Khatwaab akasema:

“Ewe Mtume wa Allah! Muamuru Abaad Ibn Bishri amuulie mbali muovu huyu”. Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-akamwambia:

“Itakuwaje ewe Umar, pale watu watakapo zungumza ya kwamba Muhammad anawaua maswahaba wake mwenyewe! Hapana asiuliwe, lakini uidhinishe msafara uanze kuondoka kwa safari ya kurejea Madinah”.

Na huu ulikuwa ni wakati ambao Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-hakuwa na mazoea ya kusafiri ndani yake; wakati wa jua kali mno.

Khabari  ya kwamba maneno aliyoyasema tayari yameshamfikia Bwana Mtume ikagonga ngoma za masikio ya msemaji; Ibn Ubayyi.

Nae akakanusha na kupinga vikali tena kwa kumuapia Allah mbele ya Mtume ya kwamba hakusema cho chote, bali anasingiziwa tu.

Bwana Mtume hakumjibu wala kumuuliza lo lote, bali aliendela na safari yake. Ibn Is-haq-Allah amrehemu-anasema: (Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alipokuwa njiani akakutana na Usayd Ibn Hudhwayr, huyu akamuamkia kwa maamkizi ya utume, kisha akasema:

“Ewe Mtume wa Allah! Wallah, kwa yakini umesafiri katika wakati mbaya ambao hukupatapo kamwe kufunga safari ndani yake!” Mtume wa Allah-Rehema na

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *