FALSAFA YA HEKIMA YA KUTAYAMAMU

Kutayamamu kumefanywa kuwa ni sheria miongoni mwa sheria za uislamu ili kumfanya muislamu aweze kuitekeleza ibada katika hali na mazingira mbalimbali yanayomzunguka.

Apate wepesi katika kulitekeleza lengo la kuumbwa kwake ambalo ni ibada kwa maana halisi ya neno hilo.

Tayamamu ni hadiya na zawadi ya Mola kwa umati Muhammad, sheria hii haikuwepo katika nyumati zilizoutangulia uma huu.

Haya yanathibitishwa na kauli ya Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie:

“Nimepewa (mambo) matano, hakupata kupewa mtume yeyote kabla yangu; Nimenusuriwa na khofu kitambo cha mwezi mzima, na nimefanyiwa ardhi kuwa ni msikiti na twahara, basi popote pale mtu katika umati wangu itakapomdiriki swala na aswali. Na nimehalalishwa ngawira na hazikuhalalishwa kwa heyote kabla yangu, na nimepewa shafaa (uombezi kwa watu). Mtume alikuwa akipelekwa kwa watu wake tu na mimi nimepelekwa kwa watu wote.” Bukhaariy na Muslim.

Itakuwazikia kutokana na hadithi hii ya Bwana Mtume kuwa kutayamamu ni fursa maalumu ya upendeleo uliyopewa muislamu na Mola wako ili kukuwepesishia utekelezaji wa ibada zako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *