Makurayshi walifanya kikao chao hiki kiovu katika mazingira na hali ya uficho na siri kuu ili kuhakikisha kuwa maamuzi yatakayofikiwa hayavuji na kuwasambaa.
Kwani hili halitamaanisha kingine zaidi ya kushindwa kwa mpango huu mzima na hivyo kumpa ushindi Mtume wa Allah.
Lakini Allah mbora wa kupindua hila za watu wabaya, mwenye khabari za lililotendeka linalotendeka na litakalotendeka kabla hata halijafikiriwa kutendwa bali kabla ya kuubwa hao watendaji
“HAKIKA ALLAH NI MJUZI WA KHABARI ZA SIRI NA KHABARI ZA DHAHIRI” ( 4.35)
“………NA ALLAH ANA KHABARI ZA YOTE MNAYOYATEDA” ( 3.153)
Akampelekkea mtume wake khabari zote za mkutano ule muovu kupitia kwa Allah imshukuru – na akampa idhini ya kuhamia Madina.
Sasa ndio Bwana Mtume akaanza kupanga mikakati ya Hijrah kwa hadhari kubwa ili asiwashitue Makurayshi.
Mtume akatambua kwamba Makurayshi wataizingira nyumba yake usiku ili kumzibia mwanya wa kutoroka.
Iwapo atafanikiwa kutoroka basi ni dhahiri kuwa wataanzisha msako wa nyumba hadi nyumba Makkah nzima, wakimkosa watamtafuta katika njia ielekeayo Madinah wataziba njia zote za kutoka Makkah ili ashindwe kutoka nje, na watafanya juhudi za makusudi ili waweze kumtia mikononi.
Wakishindwa kumkamata kwa mbinu zoote hizo , basi bila ya shaka watakataa tamaa na kuinua mikono ya kushindwa na hapo ndipo hali itarejea kuwa ya kawaida mjini Makkah.
Ni kuanzia hapo ndipo Mtume wa Allah rehema na Amani zimshukie – aakaanza kupanga mikakati yake ya kuondoka Makkah .
Akamuendea Aliy Ibn Abiny Twaalib: mwana wa Ammi yake na kumuelezea juu ya azma yake ya kuhama na akamtaka aendelee kubakia Makkah ili aweze kurejesha amana zaa watu walizomuwekea yeye mtume kwani watu wa Makkah walikuwa wakiweka kwa Bwanaa Mtume amana zao na vitu vyao vingine vya thamani kutokana na kuutambua ukweli na uaminifu wake.
Kisha huyo haraka akatoka mguu mosi mguu pili mpaka nyumbani kwa Swahibu yake Abuu Bakri – Allah amuwiye radhi ili ampe khabari ya Hijrah .
Pia amuelezee kwamba yeye ndiye rafiki mteule katika saafari hii yake ya hijrah. Kisha wapange na kuwafikianna pamoja namna na wakati wa kutoka ili safari yao usikumbanne na vikwazo vya makurayshi.
Tumpe nafasi Ibn Ishaaq – Allah amrehemu – aripoti kutoka kwa Bi. Ayshaa mkewe Mtume akisimulia namna mambo yalivyokuwa , anasema { Bi Aysha} :
“ Yalikuwa si mazoea ya Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – kuja nyumbani kwa Abuu Bakri {baba yangu } katika mojawapo ya ncha mbili za mchana {Adhuhuri na laasiri } Bali alikuwa akija ima asubuhi au Jioni.
Hata ilipofika ile siku ambayo Allah alimpa idhini ya kuhama Mtume wake . Atoke Makkah machoni mwa jamaa zake , alitujia mtume wa Allah rehema na Amani zimshukie – wakati wa jua kali la mchana , katika muda ambao hakuuzoea . {Anasema ni kumwambia :
Hakuja Mtume wa allah saa hizi ila kuna jambo tu lilitokea { Akaendelea kusema Bi. Aysha} Alipoingia, Abuu Bakri akampisha kwenye godoro lake , Mtume akakaa. Hakuwepo mtu mbele ya Abuu Bakri ila mimi na dada yangu Asmaa. Mtume wa Allah akasema “Niondoshee walioko pamoja nawe”
Akasema Abubakri
“Ewe Mtume wa Allah, hakika hawa si watu baki ila ni mabinti zangu , kwani kuna jambo gani?” {Mtume} akamwambia
“ Hakika Allah amenipa idhini ya kutoka na kuhama”. {Anasema Bi Aysha} Abu Bakri akasema :
“Tufuatane pamoja ewe mtume wa Allah” { Mtume} akamjibu :
“ Tutafuatana pamoja “ { Anaendelea kusema Bi. Aysha } Wallah sikuhisi wala kujua kabla ya siku hiyo kwamba mtu anaaweza kulia kwa furaha mpaka nilipomuona Abu Bakri siku hiyo akilia, kisha akasema “ Ewe Mtume wa Allah hakika vipando {wa nyama } viwili nilikuwa nimeviandaa tayari kwa ajili ya safari hii” Wakamkodi Abdullah Ibn Urayqitu, mtu wa kabila la Banny Duili aliyekuwa kafiri, afanye kazi ya kuwaongoza njia. Wakampa wanyama wawili wale akae nao na kuwachunga mpaka siku ya safari “ Amemalizaa kuripoti Ibn Is-Haaq.
Mpango waliopanga Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie na swahibu yake Abu Bakri ni Kutoka Makkah usiku na kwenda mpaka katika pango la “Tha uri” nje kidogo ya mji wa Makkah.
Wajifiche hapo kwa muda mpaka tafrani ya kuwatafuta itulie kabisa . Kisha ndipo watoke na kuelekea na watu.
Hivi ndivyo ulivyokuwa mpango mzima wa safari ya Mtume na Swahibu yake kuhamia Madinah , kwenda kuungana na maswala wake watu waliomkubali kwa dhati na kumtafuata kwa nia.
Wakaagana na Abdullah Ibn urayqit; mtaalamu wa njia za jangwani awafuate kati mtaalamu wa njia za jangwani awafuate katika pango la thauri baada ya siku tatu watakapotoka.
Wasifu wa Pango “ Thauri”
Thauri, hili ni pango lililopo juu ya jabali Thauri, huu ni mlima mrefu wenye vilele viwili .
Mlima huu uko umbali wa maili tatu kusini mwa mji wa Makkah katika njia ielekayo nchi ya Yemen.
Kutoka mjini Makkah mpaka katika pango hili ni mwendo wa masaa mawili kwa miguu. Pango hili liko kileleni mwa mlima huu.
Ni pango finyu lenye eneo lisilozidi mita mbili na nusu. Limelala chini ya mwamba mkubwa ambao unakuwa mithili ya paa linalilifanya pango hili kuwa na kiza cha kutisha .
Pango hili kuwa na kiza cha kutisha. Pamoja hili lina penyenye mbili zinazopatikana kwa taabu kila upande, hii ndio milango ya pango hili.
Hili ndilo pango alilijificha ndani yake Mtume wa Allah na Swahibu yake kwa muda wa siku tatu na hayo ndiyo mazingira yake.
Kwa wale watakaojaaliwa kufika katika mji mtukufu wa Makkah wanaweza kuliona pango hili.
Usiku ule
Hatimaye ukafika ule usiku uliokuwa ukisububiriwa kwa hamu na kiu kubwa sana. Bwana Mtume akiusubiri ili aweze kuitekeleza amri ya Mola wake yaa kuhamia Madinah.
Nao makurayshi kwa upande wao wakiusubiri ili waweze kuitekeleza azma yao ya kummaliza mtume wa Allah na dini yake ambayo ni tishio kwa itikadi yao ya ushirikina.
Usiku ule wale vijana shujaa , barabara wenye nguvu na wenye nia moja , wakiwa na panga kali waliizingira nyumba ya Mtume .
Wakimsubiri atoke tu, waitekeza kazi na jukumu walilopewa na desturi ya Waarabu kumuua mtu ndani ya nyumba yake.
Ally Ibn Abiy Twaalib akalala katika kitanda cha Mtume kama alivyoelekezwa na akajifunika shuka la kihadharami la rangi ya kijani la Mtume .
Ikumbukwe wakati wote huu, Bwana Mtume alikuwa angali ndani . Ulipowadia wakati wa kutoka allah akawashushia usingizi wa ajabu vijana wale walioizunguka nyumba ya Bwana Mtume .
Wakalala nao wakiwaa hawajitambui kwa usingizi . Akachukua mchanga akawanyunyuzia wote vichwani huku akisoma mwanzo mwanzo wa Suwarati Yaasin:
NA{ Kama kwamba} TUMEWEKA KIZUIZI MBELE YAO NA KIZUIZI NYUMA YAO NA TUMEWAFUNIKA { MACHO YAO} KWA HIYO HAWAONI ‘ { 36;9}
Huyoo akashika njia , akakutana na Sayyidna Abuu Bakri Mahala walipoagana kukutana . Wakaongozana mpaka katika pango la Thauri na kujificha humo.
Huku nyuma , Kulipombazuka asubuhi , vijana wale wakamuona Ally ndiye anaamka kitandani kwa Mtume .
hapo ndipo wakachanganyikiwa na kupandwa na mori wa hasira . Wakamnyakua Sayyidna Aliy , wa kimsukasuka huku na kule wakimuuliza : Yu wapi Muhammad? Ameenda wapi? Amejificha wapi Nae Imam Ally akiwajibu kwa utulivu na makini:
“ Sijui mmemshurutiza kutoka nae ametoka ” Wakaanza kumpiga , kisha wakamchukua mpaka msikitini wakamfungia humo.
Wakamkusanyikia na kutumia kila njia ili aweze kusema alipo Mtume lakini wapi hakusema .
Walipokata tamaa walimuachia na wakatawanyika pande zote za Makkaah kuanza kumsaka Bwana Mtume kwa bidii zote.
Wakaenda Mashariki na Magharibi, Kaskazini na Kusini, huku wakimuuliza kila waliyekutana naye njia . Lakini juhudi zote hizi hazikuzaa matunda.
Amepokea Ibn Is Haq – Allah amrehemu – kutoka kwa Bi Asma Bint Abiu Bakri kwamba yeye { Asma } amesema { Katika kuelezea hali iliyokuwa}
“Alipoondoka Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukiee – na Abuu Bakri – Allah amuwiye radhi – lilitujia kundi la Makurayshi akiwemo Abu Jaahli Ibn Hishaam. Wakasimaama mlangoni mwa nyumba ya Abuu Bakri , Nikawatokea , wakaniuliza : yu wapi babayo awe bint Abuu Bakri? Akasema Bi Asmaa} Nikaawajibu : Wallah ! sijui baba yangu yuko wapi. { Akaendelea kusema}: Abu Jahli akainua mkono wake na alikuwa mtu muovu mwenye maneno machafu, akanipiga kofi la nguvu lililo zidondosha chini hereni zangu.
Mtume na Swahibu pangoni:
Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie yeye na swahibu yake wakakaa pangoni mle kwa muda wa siku tatu.
Wakisikiliza khabari za vuguvugu la kumtafuta. Ibin Is–haaq anasema:
“Abdullah Ibn Bakri alikuwa akishinda na Makurayshi mchana kutwa akisikiliza mikakati wanayopanga ili kuweza kuwatia mbaroni Bwana Mtume na swahibu yake. Kisha jioni huenda pangoni kuwapasha khabari. Aamir Ibn Fuhayran – huru wa Abuu Bakri – yeye alikuwa akichunga mchana katika machungo ya watu wa Makkah. Jua likichwa huwapeleka mbuzi wa Abuu Bakri kule pangoni, wakawamua maziwa na kumchinja mmoja wakala nyama Abdullah Ibin Abuu Bakri akiondoka kule pangoni kurudi Makkah, Aamir Ibin Fuhartah alimfuatia nyuma na mbuuzi ili kuziba / kufuta athariya miguu yake. Baada ya kupita siku tatu, mtu wao waliyemuajiri akaja na ngamia wao na ngamia wake yeye tayari kwa safari”
Pamoja na ugumu wa kipindi hiki cha kutoka Makkah hadi pangoni Thauri na maisha ya pangoni mle bado Mtume alikuwa na imani thabiti juu ya ulinzi usionshindikana wa mola wake.
Hasa pale vijana wa Kikurayshi walipotumia uhodari wa kufuatilia nyayo za watu mpaka wakafika pangoni pale.
Na Abuu Bakri akawa anasikia sauti zao na mchakacho wa miguu yao. Khofu ikamtambaa Abuu Bakri, akaanza kulia ka kuona kuwa sasa maisha ya Mtume wa Allah yamo hatarini. Akasema
“Ewe Mtume wa Allah, lau mmoja wao ataangalia chini ya miguu yake, bila shaka watatuona Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – akafanya kazi ya kumtuliza Abuu Bakri na akamwambia :” Usihuzunike hakika Allah yu pamoja nasi! Unawadhaniaje wawili ambao Allah ni watatu wao?” Bukhaariy Muslim.
Qur – ani tukufu ametusajilia tukio hillo, tufuatane nayo:
“KAMA HAMTAMNUSURU {Mtume} BASI ALLAH ALIMNUSURU WALIPOMTOA WALE WALIOKUFURU; ALIPOKUWA {mmoja tu na mwenziwe} wa Pili wake {peke yao} WALIPOKUWA WOTE WAWILI KATIKA PANGO ; (Mtume) ALIPOMWAMBIA SWAHIBU YAKE : “ USIHUZUNIKE KWA YAKINI ALLAH YU PAMOJA NASI ;ALLAH AKAMTEREMSHIA UTULIVU WAKE NA AKAMNUSURU KWA MAJESHI MSIOYOYAONA (9: 40)
Majeshi aliyoyatumia Allah kumuhami, kumlinda na kumnusuru Mtume wake dhidi ya maadui hawa wenye uchu na kiu ya kumuua ni yule mdudu buibui aliyekuja akautanda utandu wake mlangoni mwa pango kwa Il-ham ya Allah.
Halafu akaja ndege akataga mayai pale . Makurayshi walipofuata nyayo na kufika pangoni walikataa katakata kuwa Mtume yumo pangoni mle wakasema .
Haiwezekani aingie pangoni humu bila ya kuvunja mayai haya na kuuharibu utandu huu. Hao wakashika njia na kwenda zao.
Baada ya kupita siku tatu , Makurayshi walikata tamaa kumpata Mtume Makkah. Wakaamua kuzielekeza juhudi na nguvu zao.
Katika njia kuu ulekeayo Madinah. Wakawatuma huko vijana wao kuendelea kumsaka Mtume wa Allah .
Wakawatangazia wakazi wote wa Pwani kwamba yeyote atakayemleta Mtume akiwa hai au amekufa atazawadiwa zawadi nono ya ngamia mia.
Habari zote hizi zikimfikia Bwana Mtumee kupitia kwa Abdallah Ibn Abuu Bakri na akazitumia kamma chanzo cha kupangia mkakati wa kutoka pangoni mle na kuanza safari ya Madinah.