HISTORIA YA ADHANA

Kwa mujibu wa kauli zenye nguvu, adhana imeshariiwa katika mwaka wa kwanza wa Hijrah.

Sababu ya kuanza kutumika kwa adhana ambayo haikuwepo katika kipindi chote cha utume Makah.

Inatajwa kwamba baada ya Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – kufika Madinah, iliwawia uzito waislamu kujua nyakati za swala.

Bwana Mtume akawataka shauri maswahaba wake wafanyeje ili swala ya jamaa isije ikawafutu.

 Baadhi ya maswahaba wakashauri ipigwe kengele kila unapoingia wakati wa swala.

Wengine wakasema lipulizwe tarumbeta (baragumu) ili kuashiria kuingia kwa wakati wa swala.

 Na pia wako waliotoa ushauri uliokhitilafina na huu, lakini katika majumuisho yote ya ushauri uliotolewa hakuna uliompendeza Bwana Mtume.

Akapendezwa na ushauri uliotolewa na Umar Ibn Al-Khatwaab – Allah amuwiye radhi.

Imepokelewa kutoka kwa Naafi, kwamba Ibn Umar Allah awawiye radhi – alikuwa akisema: Waislamu walikuwa wakikutana na kukadiria nyakati za swala na hakukuwepo ye yote anayeita kwendea swala (anayeadhini).

Siku moja wakalizungumzia suala hilo. Wakasema baadhi yao: Jifanyieni kengele kama wafanyavyo Manaswara.

Na wengine wakasema: Bali tupulize baragumu kama Mayahudi. Basi (hapo ndipo) Umar aliposema: Kwa nini hamumpeleki mtu akanadi swala?

Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – akasema:

Ewe Bilali inuka unadi swala”. Bukhaariy

Imamu Ahamd – Allah amrehemu – amepokea kwamba mmoja wa maswahaba nae ni Abdullah Ibn Zayd – Allah amuwiye radhi – alimuona malaika usingizini akamfundisha adhana na Iqaamah. (Alipoamka) akampa Mtume khabari ya ndoto yake hiyo. Mtume – Rehema na Amani zimshukie – akasema:

“Bila shaka hiyo ni ndoto ya haki (kweli) pindipo akitaka Allah, basi inuka umfundishe Bilali maneno uliyoota ndotoni nae aadhini kwayo, kwani yeye ana sauti kali kuliko wewe”.

Umar Ibn Al-Khatwaab akiwa nyumbani kwake akaisikia adhana hiyo, akatoka wanguwangu kuja kwa Mtume na kumwambia, namwapia yule aliyekutuma kwa haki, hakika nimeona usingizini haya haya aliyoyaona Abdullah Ibn Zayd”.

 

 

HISTORIA YA ADHANA

Kwa mujibu wa kauli zenye nguvu, adhana imeshariiwa katika mwaka wa kwanza wa Hijrah.Sababu ya kuanza kutumika kwa adhana ambayo haikuwepo katika kipindi chote cha utume Makah. Inatajwa kwamba baada ya Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – kufika Madinah, iliwawia uzito waislamu kujua nyakati za swala. Bwana Mtume akawataka shauri maswahaba wake wafanyeje ili swala ya jamaa isije ikawafutu. Baadhi ya maswahaba wakashauri ipigwe kengele kila unapoingia wakati wa swala. Wengine wakasema lipulizwe tarumbeta (baragumu) ili kuashiria kuingia kwa wakati wa swala.Na pia wako waliotoa ushauri uliokhitilafina na huu, lakini katika majumuisho yote ya ushauri uliotolewa hakuna uliompendeza Bwana Mtume.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *