KUTEKELEZA AHADI

Kutekeleza ahadi ni miongoni mwa tabia njema/tukufu anazotakiwa ajipambe nazo muislamu wa kweli.

Muislamu anapotoa ahadi, basi atambue kwamba amelazimishwa na sheria kuitekeleza ahadi muda wa kuwa si katika kumuasi Mola Mtukufu. Mwenyezi Mungu atuambia:-

“NA TIMIZENI AHADI. KWA HAKIKA AHADI ITAULIZWA (siku ya kiama) (17:34)

Kukhalifu au kutokutimiza ahadi ni katika jumla ya alama za unafiki wa mtu kama anavyotubainishia hilo Bwana mtume:

“Alama za mnafiki ni tatu:anapozungumza husema uwongo, na akiahidi hukhalifu (hatekelezi ahadi) na akiaminiwa hufanya khiyana”. Bukhaariy na muslimu.

Tabia ya kutekeleza ahadi humfanya mtu aaminiwe na watu, atajwe vema katika uhai na baada ya kufa kwake kama Qur-ani inavyotuambia:

“NA MTAJE KATIKA KITABU (hiki) ISMAIL. BILA SHAKA YEYE ALIKUWA MKWELI WA AHADI, NA ALIKUWA MTUME, NABII”. (19:54)

Mwenyezi Mungu amuambia Nabii Muhammad amtaje na kumkumbuka Mtume wake Ismail ndani ya Qur-ani baada ya kupita chungu ya miaka kwa sababu ya kupambika kwake na tabia tukufu ya kutekeleza ahadi.

Anayetoa ahadi na kutimiza basi atambue kwamba amepambika na sifa miongoni mwa sifa za mitume.

Sifa hii kutekeleza ahadi huambatana na sifa mbili kuu; kusema ukweli na kutokukhini amana. Basi ukimuona mtu atekeleza ahadi basi mshuhudie pia kuwa ni mkweli asiye na khiyana.

KUTEKELEZA AHADI

Kutekeleza ahadi ni miongoni mwa tabia njema/tukufu anazotakiwa ajipambe nazo muislamu wa kweli.

Muislamu anapotoa ahadi, basi atambue kwamba amelazimishwa na sheria kuitekeleza ahadi muda wa kuwa si katika kumuasi Mola Mtukufu. Mwenyezi Mungu atuambia:-

“NA TIMIZENI AHADI. KWA HAKIKA AHADI ITAULIZWA (siku ya kiama) (17:34)

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *