FALSAFA YA SWALA YA IJUMAA

Katika kushariiwa swala ya Ijumaa kuna hekima na faida kathiri (nyingi).

Katika jumla ya faida hizo ni kule kukutana waislamu katika ngazi ya mji, kitongoji au kijiji mahala pamoja.

Ambapo ni ndani ya msikiti wa Ijumaa, mara moja kila juma, mara nne kila mwezi na mara khamsini takriban kila mwaka.

Hii ni fursa muhimu na ya pekee ambayo huwaunganisha waislamu na kuzidisha nguvu yao kama ambavyo huwazidishia kuzoeana, kufahamiana na kusaidiana.

Ijumaa ni idhaa ya waislamu yenye dhima kuu ya kuwapasha waislamu matukio ya kila juma yanayojiri katika ulimwengu wao.

Idhaa hii huwanganisha waislamu na matukio haya na kuwaonyesha nafasi yao kama waislamu nyuma ya matukio hayo.

Ni kwa kiasi gani matukio hayo yanawadhuru au kuwanufaisha waislamu na wao kama waislamu wafanye nini kuyaboresha manufaa au kuyaondosha madhara yatokanayo na matukio hayo.

Ijumaa ni chuo cha nidhamu kinachowafundisha waislamu kuwa ni lazima wawe nyuma ya kiongozi wao mmoja, wakimtii na kumsikiliza katika maamrishi na makatazo, ikiwa wanataka kufaulu kama walivyofaulu maswahaba nyuma ya kiongozi wa uma; Bwana Mtume.

Ijumaa ni chuo cha usawa kinachoondosha tofauti za rangi, lugha, hadhi na hali za kimaisha baina ya waislamu.

Katika swala ya Ijumaa utamuona tajiri bilionea amekaa pembeni ya masikini hohehahe, kiongozi yuko bega kwa bega na raia wake duni, mkubwa amekaa sambamba na mdogo na hata mweupe na mweusi pia hukaa pamoja.

Hakuna nafasi maalum kwa tabaka la watu fulani, bali kila muislamu ana haki ya kukaa po pote na hakuna mwenye haki ya kumuondoa.

Ila aamue yeye mwenyewe kwa khiari yake kusogea au kumpisha nduguye muislamu, hili ni suala binafsi la matashi ya mtu. Hii ni sehemu ya falsafa kuu ya swala hii ya siku ya Ijumaa.

FALSAFA YA SWALA YA IJUMAA

Katika kushariiwa swala ya Ijumaa kuna hekima na faida kathiri (nyingi).

Katika jumla ya faida hizo ni kule kukutana waislamu katika ngazi ya mji, kitongoji au kijiji mahala pamoja.

Ambapo ni ndani ya msikiti wa Ijumaa, mara moja kila juma, mara nne kila mwezi na mara khamsini takriban kila mwaka.

Hii ni fursa muhimu na ya pekee ambayo huwaunganisha waislamu na kuzidisha nguvu yao kama ambavyo huwazidishia kuzoeana, kufahamiana na kusaidiana.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *