MGAWANYO WA MAJI KWA KUZINGATIA WINGI AU UCHACHE

Tukiyaangalia maji kwa kuuzingatia wingi na uchache wake tutayakuta yamegawanyika sehemu/mafungu mawili:-

 i/ Maji  mengi,  na
ii/ Maji  machache

i/ MAJI MENGI: Haya kwa mtazamo wa sheria ni yale yaliyofikia kullatein na zaidi yake.

Kullatein ni miongoni mwa vipimo vilivyokuwa vikitumiwa na Waarabu zamani. Kwa vipimo tuvitumiavyo leo kullatein ni sawa na lita 216 za ujazo.

Kwa vipimo vya ukubwa Kullatein ni sawa na dhiraa moja na robo upana, urefu na kina. Dhiraa moja ni sawa sawa na sentimeta 48 (48 cm)

HUKUMU YA MAJI MENGI: Maji yaliyofikia kullatein na kuendelea hayanajisiki kwa kuingia tu najisi ndani yake bali ya kuwa yamenajisika ikiwa najisi hiyo itaharibu mojawapo ya zile sifa tatu za maji.

 

ii/ MAJI MACHACHE: Maji yatahukumiwa kuwa ni machache ikiwa hayakufikia kiwango cha kullatein yaani yako chini ya lita 216 za ujazo ambazo ni karibu ya madebe 12 yaliyojaa.

HUKUMU YA MAJI MACHACHE: Maji haya yatanajisika kwa kuingiwa na najisi hata kama najisi hiyo haikuharibu mojawapo ya sifa za maji, na yatahukumiwa kwa mujibu wa sheria kuwa ni maji najisi na tayari tumekwisha itaja hukumu ya maji najisi huko nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *