KATAZO LA WIKI (JUMA LA 77)

Hivi wewe unafikiri ni nani?! Mpaka lini utaendelea kuwadhulumu na kuwanyanyasa watu, eti tu kwa sababu ya madaraka yako, cheo chako, mali yako au nguvu zako?! Kumbuka madaraka yana mwisho wake na yuko mwenye madaraka yasiyo na ukomo, cheo nacho leo ni chako na kesho ni cha mwenzako, mali nayo huja na kuondoka na hata hizo nguvu nazo hupungua siku hata siku mpaka ukarudi kwenye unyonge na udhaifu kule uliko anzia.

Kumbuka: “Wala usidhani Allah ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao. Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu”. Ibraahim [14]:42-43

Na Allah anasema: “Na lau kuwa Allah angeli wachukulia watu kwa mujibu wa dhulma zao, basi asingeli mwacha hapa hata mnyama mmoja. Lakini anawaakhirisha mpaka muda ulio wekwa. Na unapo fika muda wao hawatakawilia hata saa moja wala hawatatangulia”. An-Nahli [16]:61

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *