SUNNA ZA KUTAYAMAMU

Kumesuniwa katika utekelezaji wa tendo la kutayamamu mambo kadhaa, miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo :-

1.      Kunasuniwa katika tayamamu yale yote ambayo ni suna katika udhu. Kuanzia na :

1.      Kupiga “Bismillah” mwanzo wa kutayamamu

2.      Kuanza na sehemu ya mwanzo ya uso.

3.      Kuanza kupangusa mkono wa kulia.

4.      Kupangusa sehemu kidogo ya kichwa wakati wa kupangusa uso

5.      Kupangusa sehemu ya kufupa panya wakati wa kupangusa mikono

6.      Kufululiza baina ya kupangusa uso na mikono

7.      Kuomba dua baada ya kutayamamu.

Imepokelewa hadithi na Ammaar Ibn Yaasir- Allah awawiye radhi :

Kwamba wao walitayamamu wakiwa pamoja na Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – kwa ajili ya swala ya Alfajiri.

Wakapiga viganja vyao mchangani, kisha wakapangusa nyuso zao mara moja.

Halafu wakarudia tena kupiga viganja vyao mchangani mara nyingine, wakapangusa mikono yao yote mpaka katika maungio ya kifupa panya na bega na (kupangusa) kwapa kwa matumbo ya vitanga.Abuu Daawood

2.      Kutapanya vidole wakati wa kupiga viganja juu ya mchanga na kueneza uso kwa pigo moja tu la mchanga na kuieneza mikono kwa pigo jingine.

 

3.    Kupunguza vumbi kwa kukung’uta viganja baada ya kupiga au kwa kupulizia viganja.

Suna hii inapatikana katika hadithi iliyopokelewa na Swahaba Ibn Yaasiri- Allah amuwiye radhi – kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie alimwambia :

“Hakika si vinginevyo inakutosha kufanya hivi”. Akapiga (Mtume) viganja vyake juu ya ardhi pigo moja kasha akavikung’uta (viganja). – na katika riwaya nyingine: na akapulizia ndani yake (viganja) – halafu akapangusa kwa (viganja) hivyo.” Bukhaariy.

 

SUNNA ZA KUTAYAMAMU

Kumesuniwa katika utekelezaji wa tendo la kutayamamu mambo kadhaa, miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo :-

1.      Kunasuniwa katika tayamamu yale yote ambayo ni suna katika udhu. Kuanzia na :

1.      Kupiga “Bismillah” mwanzo wa kutayamamu

2.      Kuanza na sehemu ya mwanzo ya uso.

3.      Kuanza kupangusa mkono wa kulia.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *