Imetubainikia bayana katika somo lililotangulia kwamba makurayshi katika upinzani wao wa mtume walikuwa hawaitetei imani yao bali walikuwa wakijaribu kulinda utawala wao na maslahi yao na hatari hii ya kuanguka kwa utawala wao na kuporomoka kwa maslahi yao ndio iliyokwasukuma kuingia mapambanoni
dhidi ya uislamu wao na kiongozi wake wakajaribu kwa nguvu zao zote kumdhibiti Bwana Mtume asitoke nje ya mpaka ya Makkah kwa hofu kuenea na kutapakaa uislamu ambao waliuona kama
tishio kuu kwa utawala wa maslahi yao pamoja na udhibiti huu bado Uislamu ulifanikiwa na kupenya na kuingia Madinah, huko ukaenziwa na kupata watu walio tayari kulinda kutetea na kunusuru hata kwa gharama ya roho zao.
Kuingia uislamu kwa madinah kwa kishindo kikubwa kilibadili kabisa sura ya Madinah kutoka nchi fulani jirani rafiki na mshirika wa Makkah kuwa nchi tishio na adui mkubwa wa Makurayshi.
Makurayshi waliona hatari hii inayochungulia na wakaamua kuchukua hatua haraka za makusudi ili kukabiliana na hatari hii iliyo mbele ya macho wakaamua na kuazimia kumuua kiongozi wa hatari hiyo Bwana Mtume kabla hajainua mguu kuhamia Madinah na kwenda kuzidisha hali ya hatari inayowakabili kwani waliamini kuwa yeye ndiye kiongozi na chimbuko la vuguvugu la Uislamu.
Makurayshi walisahau kuwa Muhammad alikuwa ni mjumbe tu wa Allah na mmiliki wa Uislamu ni Allah. Kwa hiyo kuumua kwao Bwana Mtume hakutaamanisha kufa kwa Uislamu kama dini na mfumo sahihi wa maisha uliofumwa na Allah. tusome na tuone ukweli:
YEYE NDIYE ALIMLETA MTUME WAKE KA UONGOZI NA DINI YA HAKI ILI AIJALIYE KUISHINDA (dini hiyo) DINI ZOTE ITAPOKUWA WANAICHUKIA HAO WASHIRIKA”. (9:33)
Kadhalika walisahau kuwa Mtume hawezi kuuwawa kwani ana ahdi ya Allah ya kumlinda dhidi ya maadui wa da’awah:
“…. NA ALLAH ATAKULINDA NA WATU…” (5:67)
Ni kutokana na ahdi hii ndiyo Allah akamuondoshea Mtume wake rehma na amani zimshukie vitimbi na njama zote za maadui wa haki na uongofu.
Akamuandalia njia ya Hijrah kwenda Madinah na huko akamujengea na kumuwekea mazingira yote yaliyohitajika kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa da’awah.
MAKURAYSHI WALIENDELEA KUPIGA VITA UISLAMU MADINAH KAMA WALIVYOKUA WAKIPIGA VITA MAKKAH
Tayari imeshatudhihirikia kwamba Hijrah ya Mtume -Rehema na amani zimshukie –haikuwa ni kuisalimisha nafsi yake asiuliwe na Makurayshi.
Wangeweza vipi kumuua hali ya kuwa ulinzi wa Allah mshindi mwenye nguvu pamoja nae kila alipo? ni dhahiri basi Hijrah haikuwa ila kwa ajili ya da’awah, ni kwa ajili ya kupata kituo cha da’awah.
Ni kwa ajili ya kupata mazingira mazuri yatakayomuezesha kulitekeleza vema jukumu alilopewa na mola wake.
Jukumu la kusimika Uislamu ulimwenguni kote ili watu waishi kwa furaha, amani, upendo usawa na haki, ichukue nafsi ya dhulma.
Haikuingia akilini makurayshi wamnyamazie Mtume na kumuacha aishi kwa amani na akieneza Uislamu kama apendavyo, kwani kufanikiwa na kuenea kwa Uislamu maana yake ni kufa kwa muhimili wa utawala wa maslahi yao.
Vipi basi yawezekana wamuachie atulizane Madinah na kuzidi kuyahatarisha maslahi na utawala wao?
Gharama zote za mapambano na upinzani mkali wa Makkah zipotee bure bure tu, eti kwa sababu tu yuko Madinah !
Hata haiwezekani kuwachiwa hivi hivi tu wakati tayari amekwishaonekana kuwa ni hatari na kikwazo kwa misafara yao ya biashara ya kutoka na na kwenda nchi za kaskazini.
Mji wa Madinah ulikuwa ni njia kuu za misafara hii. Kwa mtazamo huu kulikuwa hakuna shaka kwamba Makurayshi watarudufisha juhudi zao katika kupambana na Uislamu ili kulinda maslahi zo na utawala wao na watafanya kila lililo katika uwezo kuwashawishi warabu wengine wajiunge nao katika kukabiliana na hatari hii (Uislamu) na hatimaye kuitokomeza kabisa.
Na hizo ndizo hatua zilizochukuliwa na Makurayshi, kwani tangu wakati huo walianzisha juhudi za makusudi za kueleza ubaya na hatari za Uislamu.
Walipeleka ujumbe wao maalumu katika makabila ya mayahudi yaliyokiua yakiishi nje ya Madinah kwa lengo la kujenga chuki baina yao na waislamu.
Kutokana na juhudi hizi mbaya, waislamu waliishi kwa khofu na tahadhari kubwa katika siku za mwanzo za maisha mapya ya Madinah wakitazamia mashambulizi wakati wowote kutoka kwa adui aliye nje ya mipaka yao na ndani.
MAKURAYSHI HAWAKUWA ADUI PEKEE WA VUGUVUGU NA HARAKATI ZA UISLAMU
Je makurayshi ndio walikuwa maadui pekee wa Uislamu wanaochukua juhudi za makusudi kuupinga n kuuzuia?
La hasha Makurayshi hawakua ndio maadui pekee au wapinzani pekee, japokuwa wao ndio waliokuwa wa mwanzo kuonyesha chuki, uadui na upinzani.
Ukweli ni kwamba makundi adui mengine mengi na haya ndio makurayshi walijaribu kuyakusanya na kuyaunganisha pamoja ili kuwa na upinzani mkali na wenye nguvu utakaorahisisha kuutokomeza Uislamu na kuumua Mtume wa Allah.
Makundi haya yalijumuisha mayahudi wengi wa Madinah na wale walioishi nje ya Madinah.
Yalikuwepo pia makundi ya wanafiki ndani ya Madinah kwenyewe na pembezoni mwake kama yalivyokuwepo makundi ya washirikina wenyeji wa Madinah na mushirikina wa makabila mengine ya waarabu. Aya ifuatayo inadhihirisha baadhi ya makundi hayo:
“NA KATIKA MAADUI WANAOKAA PEMBEZONI MWENU KATIKA VITONGOJI VYA KARIBU YENU (hapo madinah) KUNA WANAFIKI NA KATIKA WENYEJI WA MADINAH (pia kuna wengine wanafiki) WAMEBOBEA KATIKA UNAFIKI (hata) HUWAJUI (kuwa ni wanafiki) SISI TUNWAJUA TUTAWAADHIBU MARA MBILI (mara ya kwanza kwa majanga na fedheha na ya pili wakati wa kufa) KISHA WATARUDISHWA KATIKA ADHABU KUBWA” (9:101)
Makundi yote haya yalikuwa ni maadui dhahiri wa da’awah ya Uislamu, yalifanya kila juhudi kuhakikisha kuwa Uislamu unatokomezwa kabisa katika uso wa ardhi :
“… LAKINI ALLAH AMEKATAA ISIPOKUWA KUITIMIZA NURU YAKE (Uislamu) IJAPOKUWA MAKAFIRI WANACHUKIA” [9:32].
Katika upinzani na vita hivi, makundi haya adui yaligawika kimalengo. Kuna makundi ambayo lengo lililowasukuma katika mapambano huu ilikuwa ni kulinda utawala na maslahi yao yasiporwe na mfumo mpya wa maisha (Uislamu).
Kuna ambayo yalijitumbukiza vitani kwa chuki kongwe binafsi za kurithi kizazi hata kizazi. Mengine yalijikuta yakiingia mapambanoni kutokana na ushawishi wa washirika na marafiki zao.
Kadhalika yako makundi yaliyosukumwa vitani kwa hasadi na chuki ya Imani, kundi hili ndilo Allah analitaja katika kitabu chake :
“WENGI MIONGONI MWA WATU WALIOPEWA KITABU (Mayahudi) WANAPENDA WANGEKURUDISHENI NYINYI MUWE MAKAFIRI BAADA YA KUAMINI KWENU, KWA SABABU YA HUSUDA ILIYOMO MOYONI MWAO (iliyowapata) BAADA YA KUWAPAMBANUKIA HAKI …” [2:109]
MAYAHUDI WALIOPINGA UISLAMU KWA HUSDA NA MAYA
Imekwishatubainikia kwamba Makurayshi waliona Uislamu kuwa ni tishio kwa maslahi yake, hivyo walipambana nao kwa nguvu zote kwa sababu kutetea masahi yao na kulinda utawala wao.
Ama Mayahudi hili lilikua ni kundi lililoelemika lina mabaki ya mafundisho sahihi ya mbinguni. Walikuwa ni Ahlul-Kitaab walivyoita na Qurani mahala pengi:
“ENYI WATU MLIOPEWA KITABU (cha Allah, mayahudi na manasara) NJOONI KATIKA NENO LILILO SAWA BAINA YETU NA BAINA YENU; YA KWAMBA TUSIMUABUDU YOYTE ILA ALLAH WLA TUSIMSHIRIKISHE NA CHOCHOTE…….” (3:64)
Kutokana na elimu ya kitabu walivyokua nayo mayahudi ndio walitazamiwa kua watu wa mwanzo kuamini Mtume wa Allah na risala yake hii ni kwa sababu kitabu chao kilikua nikanatoa bishara ya ujio wa Nabii Muhammad sifa zake na mahali atakapoondokea.
Tena sababu ya kuja mtume haya yameelezwa wazi kua kuikamilisha taurati waliyopewa na si kuitangua:
“ENYI KIZAZI CHA ISRAEL (Nabii Yakub yaani enyi Mayahudi) ZIKUMBUKENI NEEMA ZANGU NILIZOKUPENI NA TEKELEZENI AHADI YANGU (ya kua akija Mtume mtamufata) NITATEKELEZA AHADI YENU (ya kukupeni pepo) NA NIOGOPENI MIMI TU NA AMININI NILIYOYATERREMSHA AMBAYO YANASADIKISHA YALIYO PAMOJA NANYI WALA MSIWE WA KWANZA KUKATAA…”(2:40-41)
Lakini kwa bahati mbaya Mayahudi pamoja na kutambua ukweli bado hawakua tayari kuukiri kwa sababu ya kutawaliwa na maumbile ya uchoyo na ubinafsi.
Mitume wengi walitoka katika utaifa wa israel kwa nini huyu mtume asitoke kwao na atoke kwa ndugu zao waarabu ?
Mtume huyu kuwa mwarabu nasi myahudi ni ishara ya wazi kuwa utume na utukufu unahama kwao na kwenda kwa waarabu.
Mayahudi waliitakidi kwamba wao ndio wana wa Mungu wapenzi wake na taifa lake teule na mantiki hii Mtume hawezi kutoka nje ya taifa yao:
NA MAYAHUDI NA MANASARA WANASEMA SISI NI WANA WA ALLAH NA WAPENZI WAKE” SEMA: BASI KWANINI ANAKUADHIBUNI KWA AJILI YA DHAMBI ZENU? BALI NYINYI WATU KATIKA ALIWOWAUMBA…..” (5:18)
Allah alipopeleka Mtume kutoka kwa waarabu na si mayahudi nyoyo zao zilijaa chuki na ghera zikaunguliwa kwa hasadi na mfundo.
Wakaanza kuhoji na kutilia shaka utume na dini yake wakawa wanasema huyu Muhammad siye mtume ambaye tuliyekuwa tunamtazamia na kungojea.
Wakayachoma moto maandiko matakatifu yaliyomo katika kitabu chao yanayomhusu na kumtaja Nabii Muhammad wakabadilisha maandiko yote yanayomtaja jina au wasifu na Mtume huyu na wakaanza kumchukia kumfanyia uadui na kusema:
ALLAH AMETUAHIDI YA KUWA TUSIMUAMINI MTUME YEYOTE MPAKA ATULETEE KAFARA MBAYO HULIWA NA MOTO….” (3:183)
Walikusudia kumfanya mtume ashindwe na hivyo kubatilisha utume wake.
Wakaongozwa na hasadi hii kuupiga vita uislamu kwa nguvu zao zote mpaka kudhihiri katika uso wa ardhi dini nyingine ila dini yao tu.
Mtume aliutambua uadui huu lakini pamoja na hayo aliwalingania Uislamu kwa upole, ulaini na hoja, akiwambia :
“ENYI WATU MLIOPEWA KITABU (cha Allah, Mayahudi na Manswara)! NJOONI KATIKA NENO LILILO SAWA BAINA YETU NA AINA YENU; YA KWAMBA MUISIMUABUDU YEYOTE ILA ALLAH, WALA TUSIMSHIRIKISHE NA CHO CHOTE, WALA BAADHI YETU TUSIWAFANYE WENGINE KUWA WAUNGU BADALA YA ALLAH …” [3:64].
Na akiwasuta kwa upole na ulaini pia :
“SEMA : ENYI WATU MLIOPEWA KITABU ! KWA NINI MNZAIKATAA HOJA ZA ALLAH, HALI ALLAH NI SHAHIDI JUU YA YOTE MNAYOTDENDA ? SEMA : ENYI MLIOPEWA KITABU! KWANINI MNAWAZUILIA (watu) NA NJIA (dini) YA ALLAH WALE WALIOAMINI ? MKAITAFUTIA KOSA, NA HALI MNASHUHUDIA (kuwa ni njia ya Allah isiyokuwa na kosa ) NA ALLAH SI MWENYE KUGHAFILIKA NA MNAYOTENDA “ [3:98-99].
Na akiwakumbusha neema ya Allah juu yao na wito wake kwao :
“ENYI KIZAZI CHA ISRAILI (Nabii Yaaqub ! Yaani Enyi Mayahudi !) ZIKUMBKENI NEEMA ZANGU NILZOKUNEEMESHENI; NA TEKELEZENI AHADI YANGU (ya kuwa akija Mtume mtamfuata) NITAITEKELEZA AHADI YENU (ya kukupeni pepo) NA NIOGOPENI MIMI TU. NA AMININI NILIYOYATEREMSHA AMBAYO YANASADIKISHA YALIYO PAMOJA NANYI, WALA MSIWE WA KWANZA KUYAKATAA. WALA MSIYAUZE MANENO YANGU KWA AJILI YA THAMANI NDOGO TU (ya kilimwengu) NA NIOGOPENI MIMI TU. WALA MSICHANGANYE HAKI NA BATILI, NA MKAFICHA HAKI NA HALI MNAJUA. NA SIMAMISHENI SWALA (Enyi Mayahudi) NA TOENI ZAKA NA INAMENI PAMOJA NA WANAOINAMA (yaani kuweni Waislamu) JE, MNAWAAMRISHA WATU KUTENDA MEMA NA MNAJISAHAU NAFSI ZENU, HALI MNASOMA KITABU (cha Allah kuwa kufanya hivyo ni vibaya) ? BASI JE, HAMFAHAMU ?” [2:40-44].