Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifia sana waja wake wanapenda kujitwaharisha na kujitakasa ndani ya Qur-ani aliposema:
“HAKIKA ALLAH HUWAPENDA WANAOTUBU NA HUWAPENDA WANAOJITAKASA”. (2:222)
Utaona kutokana na aya hii kwamba twahara ni sababu ya kuyavuna mapenzi ya mola Mwenyezi. Mwenyezi Mungu anazidi kutuonyesha ubora wa twahara kwa kusema:
“MSIKITI ULIOJENGWA JUU YA MSINGI WA KUMCHA ALLAH TANGU SIKU YA KWANZA (ya kufika Mtume Madinah) UNASTAHIKI ZAIDI WEWE USIMAME HUMO. HUMO WAMO WATU WANAOPENDA KUJITAKASA NA ALLAH ANAWAPENDA WAJITAKASAO”. (9:108)