ADHANA ISIYO YA SWALA

Kumesuniwa kutolewa adhana pindi kutakapotokea katika jamii ya waislamu mambo kadhaa mbali ya swala. Mambo hayo yaliyosuniwa adhana ni pamoja na:-

Kumuadhinia mtoto katika sikio lake la kulia mara tu baada ya kuzaliwa, kama ambavyo ni suna kuleta iqaamah katika sikio lake la kushoto.

Suna hii inatokana na kitendo cha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-kumuadhinia sikioni mjukuu wake; Hassan alipozaliwa na Bibi Faatimah (bintiye). Riwaya hii ameipokea imamu Tirmidhiy

Adhana wakati linapotokea janga la moto. Falsafa ya adhana hii ni kuwaita waislamu kuja kutoa msaada wa uokozi na kuzima moto.

Adhana wakati wa vita. Falsafa ya adhana hii ni kuwakusanya waislamu kwa lengo la kwenda vitani kuihami dini ya Allah.

Kumuadhinia mtu aliyeanguka mweleka, mtu aliyeghadhibika mno, mtu mwenye tabia mbaya na mtu aliyesibiwa/aliyekumbwa na shetani wa kijini.

Falsafa ya adhana hii ni kuwaondoshea shari watu hawa kwa utajo huu wa Allah, hii ni kwa sababu shetani hukimbia mbali anapoisikia adhana.

ADHANA ISIYO YA SWALA

Kumesuniwa kutolewa adhana pindi kutakapotokea katika jamii ya waislamu mambo kadhaa mbali ya swala. Mambo hayo yaliyosuniwa adhana ni pamoja na:-

Kumuadhinia mtoto katika sikio lake la kulia mara tu baada ya kuzaliwa, kama ambavyo ni suna kuleta iqaamah katika sikio lake la kushoto.

Suna hii inatokana na kitendo cha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-kumuadhinia sikioni mjukuu wake; Hassan alipozaliwa na Bibi Faatimah (bintiye). Riwaya hii ameipokea imamu Tirmidhiy

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *