KUZALIWA KWA BWANA MTUME

Bwana Mtume – Allah amshushie rehma na amani – alizaliwa katika mji wa Makkah, siku ya Jumatatu mwezi wa mfungo sita, mwaka wa tembo sawa na tarehe 20 ya mwezi April mwaka 571 – Miyladia (tangu kuzaliwa Nabii Issa).

Bwana Mtume alizaliwa hali ya kuwa ni yatima kwani baba yake alikufa akimuacha mkewe ana mimba ya Mtume.

Mama yake alipojifungua tu alimpeleka mjumbe kwa babu yake Mtume Mzee Abdul -Mutwalib kumpa khabari njema za kuzaliwa mjukuu wake. Mzee Abdul – Mutwalib akafurahikia sana mjukuu wake akamchukua na kumzungusha katika Al-Kaaba na akamuita Muhammad.

Tumesema Bwana Mtume amezaliwa mwaka wa tembo. Qur-ani Tukufu imeuzungumza mwaka huu katika sura maalum iliyoitwa kwa jina la Suuratul –Fiyl (Sura ya tembo).

Kisa cha mwaka wa tembo kinaanzia pale Abraha mfalme wa Habashah na Yaman alipowaona Waarabu wakihiji Makkah na ibada hii ya Hijjah ikaufanya mji wa Makkah kuwa ni kitovu cha biashara .

Mfalme Abraha akadhamiria kuihamisha ibada hii ya Hijjah kutoka Makkah na kuipeleka katika milki ya himaya yake ya Yaman.

Ili kuutekeleza mkakati wake huu akajenga kanisa kubwa sana na kulipamba kwa mapambo ya fakhari ili watu wavutike na kuja kufanya ibada ya Hijjah hapo.

Baada ya ujenzi huo, akawaamrisha watu waje kuhiji hapo, amri hii ikawa nzito kwa Waarabu kuitekeleza na hawakuiridhia.

Ili kuonyesha chuki yao dhidi ya amri hii alitoka mtu mmoja wa kabila ya kinaanah akaja kufanya haja kubwa ndani ya kanisa lile.

Kitendo hiki cha kulichafua kanisa kilimkasirisha sana Mfalme Abraha, hasa baada ya kugundua kwamba mhusika wa kitendo hicho ni mtu kutokea pande za Makkah.

Akaandaa jeshi kubwa lililokuwa limesheheni tembo wengi ili kwenda kuivunja Al-kaaba na yeye mwenyewe alikuwa amempanda tembo mkubwa sana kuliko wote.

Waarabu wa Makkah waliogofya sana na jeshi lile. Jeshi la Abraha lilipofika katika viunga vya mji wa Makkah likawakuta ngamia, kondoo na mbuzi wa watu wa Makkah na wengine walikuwa ni milki ya babu yake Mtume Mzee Abdul-Mutwalib, Abraha awachukua wanyama wale wote.

Mzee Abdul-Mutwalib kiongozi wa kabila la Kikurayshi, mtumishi wa Al-Kaab na mtawala wa Makkah akamuendea Abraha na kumtaka amrejeshee wanyama wake aliowachukua Abraha akamshangaa sana Mzee Abdul – Mutwalib akamwambia:

“Mimi nilitazamia umekuja kuniomba nisiivunje Al-Kaab, kumbe umekuja kunitaka nikurudishie wanyama wako!” Mzee Abdul – Mutwalib akamjibu:

“Mimi wa kwangu ni hawa wanyama, ama hii nyumba yupo mwenyewe atayeihami”.

Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu alishushia jeshi la Abraha jeshi la ndege wanaolidondoshea jeshi la Abraha mawe kutoka motoni.

Jiwe likimpata mtu anasagikasagika yeye na tembo wake na kuwa kama majani yaliyoliwa na wadudu kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani.

Tokea hapo Waarabu wakawa wanaitaja kalenda yao kwakuinasibisha na tukio hili kubwa na hii ndio maana tunasema Bwana Mtume alizaliwa mwaka wa tembo.

KUZALIWA KWA BWANA MTUME

Bwana Mtume – Allah amshushie rehma na amani – alizaliwa katika mji wa Makkah, siku ya Jumatatu mwezi wa mfungo sita, mwaka wa tembo sawa na tarehe 20 ya mwezi April mwaka 571 – Miyladia (tangu kuzaliwa Nabii Issa).

Bwana Mtume alizaliwa hali ya kuwa ni yatima kwani baba yake alikufa akimuacha mkewe ana mimba ya Mtume.

Mama yake alipojifungua tu alimpeleka mjumbe kwa babu yake Mtume Mzee Abdul -Mutwalib kumpa khabari njema za kuzaliwa mjukuu wake. Mzee Abdul – Mutwalib akafurahikia sana mjukuu wake akamchukua na kumzungusha katika Al-Kaaba na akamuita Muhammad.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *