MKATABA BAINA YA MTUME NA MAYAHUDI

Tumeona kwamba miongoni mwa wakazi wa Madinah yalikuwemo makundi ya Mayahudi.

Mayahudi hawa walikuwa si watu wa kupuuzwa hata kidogo, kwani walikuwa na nguvu za kijeshi na kiuchumi, Bwana Mtume alilitambua vema hili.

Kwa upande wa kijeshi mayahudi walikuwa na ngome imara zilizouzunguka miji yao huku ikilindwa na askari mahiri wenye zana bora na za kutosha.

Qur-ani Tukufu inazitaja ngome zao hizi na nguvu yao:

“YEYE NDIYE ALIYEWATOA WALIOKUFURU MIONGONI MWA WATU WA KITABU (Mayahudi wa Kibanin-Nadhwir) KATIKA NYUMBA ZAO (huko Madinah); WAKATI WA UHAMISHO (wao) WA KWANZA. HAMKUDHANI YA KUWA WATATOKA (kwa nguvu zao walizokuwa nazo Madinah) NAO WALIDHANI KUWA NGOME ZAO ZITAWALINDA NA (kufikwa na amri ya) ALLAH, LAKINI ALLAH ALIWAJIA KWA MAHALA WASIPOPATAZAMIA, NA AKATIA WOGA KATIKA NYOYO ZAO (wasiweze kupigana na waislamu walipokuja kupigana nao)…” [59:2]

Kwa nyanja ya uchumi mayahudi walimiliki mashamba makubwa na asilimia kubwa ya biashara.Mayahudi wa Baniy Qayunqaa waliishi katika kitovu cha mji wa Madinah wakijishughulisha na kazi ya usonara. Kadhalika walimiliki soko kuu mjini Madinah.

Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie- aliiona hatari hii ya ndani inayoukabili Uislamu. Akaamua kutumia siasa ya ujirani mwema na amani ili apate amani ya ndani, itakayomsaidia kupambana na adui wa nje.

Mtume akaanzisha mazungumzo ya amani baina yake na mayahudi, akajitahidi sana kutumia lugha ya kirafiki na maridhiano na kuustahamilia ufedhuli na ujeuri wao.

Akajikurubisha sana kwao kwa kushirikiana nao katika baadhi ya matukufu ya dini yao ambayo hayakhalifiani na Uislamu.

Akajumuika nao katika swaumu ya Ashuraa waliyokuwa wakiiadhimisha kila mwaka. Swahaba wa Mtume, Ibn Abbas-Allah amuwiye radhi-anatuambia kuhusiana na swaumu hii ambayo asili (chimbuko) yake ni mayahudi anasema:

“Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alipofika Madinah aliwakuta mayahudi wakifunga siku ya Ashura(mwezi 10 Muharram). Mtume akawauliza: Ni siku gani hii muifungayo? Wakamjibu: Hii ni siku tukufu, ni siku ambayo Allah alimuokoa Musa na watu wake na kumgharikisha Fir-aun na jeshi lake. Musa aliifunga siku hii kwa kumshukuru Allah, na sisi ndio tunaifunga (kuadhimisha tukio hilo). Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-akasema: Sisi tuna haki zaidi (ya kumfuata Musa) kuliko nyinyi, Mtume akaifunga (siku hiyo) na akawaamrisha maswahaba wake kuifunga”. Bukhaariy & Muslim.

Kadhalika wakati wa swala Bwana Mtume alielekea Baytil-Maqdis (Jerusalem) kama walivyokuwa wakielekea wao. Akaheshimu uhuru wao wa kuabudu kwa mujibu wa taratibu na sheria za dini yao. Akaheshimu haki yao ya kuishi na kumiliki mali.

Akawafungulia wazi mlango wa ushirikiano katika kuuhami mji wao wa Madinah dhidi ya maadui wa nje.

Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-aliyafanya yote haya kwa lengo la kujenga mazingira ya uhusiano bora na hali ya kuaminiana ili amani itawale Madinah.

Lakini wapi, mayahudi ni mayahudi tu hata ukiwafanyia nini! Juhudi hizi za Bwana Mtume zikawa kama mavumbi yapeperushwayo na upepo na mayahudi wakaziona kama ni njia ya Bwana Mtume kutaka kujipendekeza kwao.

Moto wa hasadi ya kuhama utume kutoka kwao na kwenda kwa waarabu ulikuwa ukiwaka nyoyoni mwao.

Mbele yao kulikuwa hakuna maji ya kuuzima moto huo ila ni kwa waislamu kurejea ukafirini baada ya kupata neema ya Imani (Uislamu).

Likawa lengo lao na lengo la mushrikina ni moja; kuutokomeza Uislamu, Allah anawataja mayahudi na wenzao mushrikina:

“HAWAPENDI WALIOKUFURU MIONGONI MWA WATU WALIOPEWA KITABU (nao ni mayahudi na manaswara) WALA WASHIRIKINA, MTEREMSHIWE KHERI KUTOKA KWA MOLA WENU. NA ALLAH HUMTEREMSHIA REHEMA ZAKE AMTAKAYE NA ALLAH NI MWENYE FADHILA KUBWA KABISA”. [2:105]

“HAWATAKUWA RADHI JUU YAKO MAYAHUDI WALA MANASWARA MPAKA UFUATE MILA YAO…” [2:120]

Moto huu wa hasadi na uadui ukazidi kuwaka pale walipoona nguvu ya Mtume inarudufika na dini yake kudhihiri na kuenea.

Hapo sasa wakashindwa tena kujimiliki na kuidhibiti chuki na uadui waliouficha nyoyoni mwao.

Wakaianika wazi hasadi yao dhidi ya Mtume na Uislamu, wakaanza kumfanyia vitimbi namna kwa namna. Mtume akaamua kuchukua juhudi za mwisho ili kuhakikisha kuwa kuna maridhiano na hali ya maelewano baina yao. Akaandikiana nao mkataba wa amani ambao ulilenga:

q       Kuacha vita na uadui baina yao.

q       Kuacha kushirikiana na maadui wa pande mbili hizo dhidi ya upande mmoja.

q       Kupigana bega kwa bega na ye yote atakayeishambulia Madinah.

q       Kila mmoja aabadu kwa mujibu wa imani yake bila ya kubughudhiwa.

Haya ndiyo yaliyokuwemo ndani ya mkataba huu wa amani baina ya Mtume na mayahudi wasio na ahadi. Je, mayahudi waliuheshimu mkataba huu? Endelea kufuatana nasi katika mfululizo wa darasa hizi ili upate jawabu kaafi ya swali hili.

 

WANAFIKI WALIDHIHIRISHA UISLAMU NA KUFICHA UADUI WAO.

Wanafiki ni wale ambao husema wameamini kwa vinywa vyao na ilhali nyoyo zao zimebakia katika ukafiri.

Hawa huswali kama wanavyoswali waislamu, hufunga kama wanavyofunga waislamu. Hushirikiana pamoja na waislamu katika matukufu ya kidini, wao katika sura ya nje ni waislamu safi tena wakereketwa.

Lakini batini yao imeficha chuki na uadui dhidi ya Uislamu na waislamu. Hii ndio Qur-ani Tukufu na sura ya wanafiki:

“NA KATIKA WATU WAKO (wanafiki) WASEMAO: TUMEMUAMINI ALLAH NA SIKU YA MWISHO, NA HALI YA KUWA WAO SI WENYE KUAMINI.WANATAFUTA KUMDANGANYA ALLAH NA WALE WALIOAMINI, LAKINI HAWADANGANYI ILA NAFSI ZAO, NAO HAWATAMBUI. NYOYONI MWAO MNA MARADHI, NA ALLAH AMEWAZIDISHIA MARADHI. BASI WATAKUWA NA ADHABU IUMIZAYO KWA SABABU YA KULE KUSEMA KWAO UWONGO”. [2:8-10]

Hili ni kundi hatari sana ni mithili ya chui aliyejivisha ngozi ya mwanakondoo ndani ya kundi la wanakondoo.

Hatari yao inatokana na kule kujichanganya kwao na waislamu wakajipamba na mapambo na matendo ya dhahiri ya Uislamu, kiasi cha kushindwa kuwatambua wawapo pamoja na waumini. Hili analithibitisha Allah ndani ya Qur-ani:

“…NA KATIKA WENYEJI WA MADINAH (pia kuna wengine wanafiki) WAMEBOBEA KATIKA UNAFIKI (hata) HUWAJUI (kuwa ni wanafiki) SISI TUNAWAJUA. TUTAWAADHIBU MARA MBILI, KISHA WATARUDISHWA KATIKA ADHABU KUBWA”. [9:101]

Kutokana na ukubwa wa hatari yao, Allah amewaandalia pia adhabu kubwa na kali:

“BILA SHAKA WANAFIKI WATAKUWA KATIKA TABAKA YA CHINI KABISA KATIKA MOTO. HUTAMKUTA KWA AJILI YAO MSAIDIZI (yo yote)”. [4:145]

Kwa nini wanafiki walikuwa na chuki kwa Uislamu na waislamu? Yalikuwepo makundi mengi ya wanafiki, lipo kundi lililoubughudhi Uislamu kwa kuona kuwa Uislamu unalikosesha manufaa na maslahi yake kutokana na sera ilizoleta.

Lilikuwepo pia kundi lililouona Uislamu kama ni tishio na hatari kuu dhidi ya dini yao. Yaani mfumo wao wa maisha unaofuata itikadi za kishirikina.

Pia lilikuwepo kundi lilouchukia na kuupiga Uislamu vita vya ndani kwa ndani kutokana na kusikiliza propaganda za mayahudi, zilizolenga kuupaka matope na kuutia dosari Uislamu.

 Kadhalika lilikuwepo kundi ambalo lilikuwa na chuki binafsi, hili lilimuona Mtume na maswahaba wake kama ni wahamiaji haramu waliokuja kuharibu mila na tamaduni zao.

Hivyo ni lazima watumie mbinu za makusudi kuhakikisha kuwa Mtume na maswahaba wanarudi kwao.

Makundi yote haya ya wanafiki yalikuwa yakitazamia ushindi wa Uislamu dhidi ya mayahudi, washindani wao wakuu.

Wanafiki walipoona Uislamu unazidi kupata nguvu siku hata siku, wakajiingiza katika Uislamu ili wapate kichaka cha kujificha na kuuhujumu Uislamu bila kujulikana.

Wakafanikiwa kujipenyeza na kuingia katika safu za waislamu na kupata fursa ya kujua siri za waislamu na kuziuza kwa maadui.

Kwa mtindo huu, wanafiki wakawa ni hatari zaidi kwa waislamu kuliko mayahudi na mushrikina.

Kundi hili la wanafiki liliongozwa na Abdullah Ibn Ubayyi Ibn Saluul. Wataalamu wa mambo ya Sira na Tarekh (historia) wanaeleza sababu iliyomsukuma mtu huyu kuuchukia Uislamu na kuamua kuliongoza kundi hili pinzani, kundi hatari sana, wanasema:

“Hakika Abdullah Ibn Ubayyi Ibn Saluul ndiye aliyekuwa kiongozi wa wanafiki. Sababu iliyompelekea kuufanyia uadui Uislamu ni kwamba wazalendo wa Madinah; Ausi na Khazraji walitaka kumtawaza ufalme ( awe mfalme wao).

Hili likipangwa kutekelezwa na wakati huo huo ndio Mtume-Rehema na Amani zimshukie-akawasili Madinah.

Walipomuamini Mtume na kuisadiki da’awah yake, walilitupilia mbali lile suala la kumtawaza Abdullah Ibn Ubayyi na wakauelekeza utii wao wote kwa Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie.

Jambo hili likaweka mfundo katika nafsi ya Abdullah Ibn Ubayyi na akawa anamtazama Mtume wa Allah kwa jicho la chuki.

Chuki hii ikamsukuma kutokumuamini Mtume, akaendelea kubakia na imani yake ya kishirikina mpaka pale waislamu walipopata ushindi mkubwa katika vita vya Badri mnamo mwaka wa pili wa Hijrah.

Alipoona Uislamu unazidi kupata ushindi na kuenea kwa kasi ya kutisha, akawaambia wafuasi wake: “Hii sasa ndio fursa”.

Hapo ndipo walipojiingiza ndani ya Uislamu kwa lengo la kuuhujumu kwa ndani na bila ya kujulikana upesi.

 

MKATABA BAINA YA MTUME NA MAYAHUDI

Tumeona kwamba miongoni mwa wakazi wa Madinah yalikuwemo makundi ya Mayahudi.

Mayahudi hawa walikuwa si watu wa kupuuzwa hata kidogo, kwani walikuwa na nguvu za kijeshi na kiuchumi, Bwana Mtume alilitambua vema hili.

Kwa upande wa kijeshi mayahudi walikuwa na ngome imara zilizouzunguka miji yao huku ikilindwa na askari mahiri wenye zana bora na za kutosha.

Qur-ani Tukufu inazitaja ngome zao hizi na nguvu yao:

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *