HISTORIA YA DINI

Baada ya kuiangalia kwa mukhtasari dhana na maana ya dini, hebu sasa tujiulize dini imeanzia wapi?

Tukiichukulia dini kwa maana ya aina Fulani ya mfumo wa maisha uliochaguliwa na kufuatawa na Jamii Fulani ya wanadamu.

Tutagundua kwamba historia ya dini inaenda sambasamba na historia ya kuanza kuwepo kwa mwanadamu katika maisha ya ulimwengu huu.

Hili ni dhahiri kwa sababu hakuna mwanadamu aliyepata kuishi, anayeishi au atakayeishi katika ulimwengu huu bila ya kufuata mfumo maalumu wa maisha.

Iwe ni mfumo alio na khiyari nao mithili ya hizo mila/desturi, ujamaa, ubepari, ukomunisti na kadhalika.

Au ule asio na khiyari nao mithili ya ule utaratibu mzima wa tangu kutungana kwa mimba, kuzaliwa mpaka kufa na yote yahitajikayo ili kuukamilisha utaratibu huu.

Kwa mantiki hii basi huu unakuwa ni ushahidi wa kimazingira unaoonyesha kuwa dhana dini imeanza kuishi sambasamba na mwanzo wa kuwepo kwa mwanadamu katika ulimwengu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *