NGUZO ZA KUTAYAMAMU

Nguzo za tayamamu, haya ni mambo ya msingi kabisa mabayo kuwepo / kupatikana kwa tayamumu kunayategemea, na haya ni mambo yanayofanyika ndani ya tayamamu yenyewe. Mambo yenyewe ni kama yafuatavyo:  

1.      Nia: Hii ndiyo nguzo ya kwanza na ya msingi ya tayamamu. Anuie moyoni mwake kuondosha hadathi ndogo au hadathi kubwa.

2.      Kupaka (vumbi) uso wote na mikono mpaka vifundoni kwa mapigo mawili.

Nguzo hii hutekelezwa kwa kupiga viganja juu ya fungu la mchango twahara wenye vumbi na kuupaka za uso kwa vumbi lililomo kwenye viganja hivyo.

Kisha vipigwe viganja kwa mara ya pili juu ya lile fungu la pili la mchanga na kuipakaza mikono hadi vifundoni kwa vumbi lililomo viganjani.

Haya ni kwa mujibu wa hadithi iliyopokelewa na Ibn Umar-Allah amuwiye radhi – amesema : Amesema Mtume – Rehema na Amani zimshukie

“ Tayamamu ni mapigo mawili, pigo moja ni la uso na pigo jingine ni la mikono mpaka vifundoni” Daaruqutwniy.

ZINGATIA: Ni lazima mtu ahakikishe kiungo chote cha tayamamu, ambacho ni uso na mikono, kimeenea vumbi kama kinavyoenea maji katika kutawadha.

Iwapo amevaa pete kidoleni, basi itamuwajibikia kuivua wakati wa pigo la pili ili vumbi liweze kufika mahala hapo.

3.      Utaratibu: Hii ndiyo nguzo ya mwisho ya tayamamu.

Mtu aanze kutayamamu kwa kupangusa uso na amalizie na kupangusa mikono hadi vifundondoni.

Hii ni kwa sababu tayamamu ni badala ya udhu, na utaratibu ni nguzo miongoni mwa nguzo za udhu kama ulivyokwisha jifunza katika masomo yaliyopita.

Kwa mantiki hii utaratibu unakuwa ni nguzo katika tayamamu ambayo ni badala ya udhu.

NGUZO ZA KUTAYAMAMU

Nguzo za tayamamu, haya ni mambo ya msingi kabisa mabayo kuwepo / kupatikana kwa tayamumu kunayategemea, na haya ni mambo yanayofanyika ndani ya tayamamu yenyewe. Mambo yenyewe ni kama yafuatavyo:  

1.      Nia: Hii ndiyo nguzo ya kwanza na ya msingi ya tayamamu. Anuie moyoni mwake kuondosha hadathi ndogo au hadathi kubwa.

2.      Kupaka (vumbi) uso wote na mikono mpaka vifundoni kwa mapigo mawili.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *