DINI

Kila sikio la mwanadamu aliyewahi kuishi, anayeishi na atakayekuja kuishi katika ulimwengu huu limepata kulisikia, linasikia na litalisikia neno “dini”. Neno hili “dini” neno fupi Kabisa, neno lenye herufi nne tu, d+i+n+i ni neno hai au tunaweza kusema ni neno linalobeba dhana hai iishiyo sambamba na mwanadamu. Ni sawasawa mwanadamu analitambua hilo au halitambui au anajitia kutokulitambua, kwani kule kutokuitambua kwake hakuondoshi/hakufuti ukweli kuwa yeye na dini ni washirika pacha katika maisha haya. Kwa hiyo basi neno hilo fupi na jepesi mno kutamka ulimini “dini” lina athari kubwa katika maisha ya kila siku ya mwanadamu na ulimwengu wake kwa ujumla. Athari hiyo inaweza ama kuwa nzuri au mbaya kutegemeana na ufahamu/uelewa wa mwanadamu kuelekea dhana hii dini.

One thought on “DINI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *