WITO WA SWALA ZISIZO ZA FARADHI

Imethibiti kutokana na maelezo yetu yaliyotangulia kwamba adhana na iqaamah ni suna zilizokokotezwa (Muakadah) kwa swala za fardhi.

Ama swala nyingine zisizo za fardhi na ambazo zimesuniwa kuswaliwa jamaa mithili ya swala za Eid mbili (Eid ya mfunguo mosi baada ya Ramadhan na ile ya mfunguo tatu baada ya hijjah).

 Swala za jua kupatwa na mwezi na mwezi kupatwa na jua na swala ya jeneza. Hizi hazikusuniwa ndani yake adhana wala iqaamah, bali wito wake ni mtu kusema:

AS-SWALAATU JAAMI’AH.

Imepokewa kutoka kwa Abdullaah Ibn Amrou-Allah amuwiye radhi-amesema: Wakati jua lilipopatwa katika zama za Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-kulinadiwa: As-swalaatu jaami’ah”. Bukhaairy & Muslim

Ichukuliwe swala hii ya kupatwa kwa jua kama mizani ya kupimia swala nyingine za suna zilizosuniwa kuswaliwa jamaa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *