MAAGANO YA PILI YA AQABAH

Msimu uliofuatia wa Hijjah, Uislamu ulikuwa tayari umeenea kwa kiasi kikubwa katika mji wa Yahrib (Madinah).

Katika kundi kubwa la Mahujaji kutoka Yathrib lililowajumuisha pamoja waislamu na mushrikina, walikuwemo waislamu sabini na tatu, miongoni mwao wakiwemo wanawake wawili. Mtume Rehema na Amani zimshukie akapanga kukutana na ujumbe huu kutoka Yathrib “Aqabah” usiku.

Akawaagiza kutokufanya harakati zozote zitakazowafanya mushrikina waliokuja nao kuhisi kitu. wasije kama kundi, bali mtu mmoja mmoja au wawili wawili na waje baada ya kupita theluthi ya kwanza ya usiku yaani baada ya saa nne usiku na kwamba wasimsubiri asiyepo na wala wasimuashe aliyelala.

Swahaba Kaa’abu Ibn Maalik Allah amuwiye radhi, analisimulia tuko hili zima la maagano ya pili ya “Aqabah”, anasema: —

Kisha tukatoka kwenda kuhiji na tukaagana na Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie kukutana “Aqabah” katika masiku ya kuanika nyama {Ayyaamut tashriyq}.

Tulipomaliza kuhiji, na ukawa uwewadia ule usiku wa maagano yetu na Mtume wa Allah. Akaendela kusema:

Usiku ule tukalala pamoja na jamaa zetu katika makambi yetu mpaka ilipopita theluthi ya usiku. Tukatoka makambini mwetu kwenda katika maagano yetu na Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie.

Tukatoka kwa uficho mkubwa mpaka tukakutana na Mtume pale “Aqabah” nasi tukiwa watu sabini na tatu pamoja na wanawake wawili.

Akaendelea kusema: Tukakusanyika pale tukimngojea Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie mpaka alipotujia akiwa pamoja na ami yake Abbaas Ibn Abdul Mutwallib.

Wakati huo alikuwa bado hajasilimu, ila alipendelea tu kuhudhuria suala la mwana wa nduguye. Mtume alipokaa, mzungumzaji wa mwanzo akawa ni Abbaas, akasema:

“Enyi kusanyiko la Khazraji, bila shaka mnatambua Muhammad alivyo kwetu. Sisi tumemkinga na madhara ya ndugu zetu wenye msimamo kama wetu kwake.

Kwa hiyo yeye anaishi katika utukufu wa jamaa/ndugu zake na ulinzi katika nchi yake. Nae ameyakataa yote hayo na kutaka kujumuika na kujiunga nanyi.

Sasa iwapo nyinyi mnaona mnaweza kumtekelezea mnayomuitia na mtamlinda dhidi ya wapinzani wake, basi hilo ni jukumu lenu mnalibeba.

Na ikiwa nyinyi mnaona mtamsaliti na kuacha kumnusuru baada ya kwenda nae huko kwenu, basi muacheni kuanzia sasa hivi”. Baraau Ibn Al-ma’aruwr (akasimama) na kusema: “Hakika sisi, wallah! Lau lingekuwemo mioyoni mwetu tusilolitamka basi tungelilisema tu, sisi tunachotaka ni ukweli na utekelezaji ahadi na kumwaga damu zetu kwa ajili ya Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie sema tu ewe Mtume wa Allah, shurutiza ulitakalo kwa nafsi yako na kwa ajili ya Mola wako, nasi tutakupa ahadi ya utii.”

Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie akazumgumza kwanza akawaraghibishia uislamu, halafu ndipo akasema:

“Nipeni ahadi kuwa mtanisikiliza na kunitii na mtaamrisha mema na kukataza maovu. Mtailingania dini ya Allah bila kuogopa lawama ya anayewalaumu na kwamba mtaninusuru na kunilinda nitakapokuja kwenu, kama mnavyojilinda wenyewe, wake zenu na wana wenu, nanyi mtapata pepo.”  Akaendelea kusema:

Baraau Ibn Al-ma’aruwr akaushika mkono wake (Mtume) na kusema:

“Naam, ninamuapia yule aliyekutuma kwa haki, fanya maagano nasi, wallah sisi ni wana wa vita na watu wa silaha, haya tumeyarithi kizazi hadi kizazi.

Akaendela kusema: Abul-haytham Ibn Tayihaan akamkata kauli Baraau, akasema:

Ewe Mtume wa Allah, hakika sisi tuna ahadi/mkataba na mayahudi, nasi tunaivunja kwa ajili yako.

Sasa isije ikawa huku sisi tumevunja ahadi, nawe Allah akakupa ushindi, ukarejea kwenu na kutuacha! Akasema: Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie akatabasamu na kusema:

“Bali damu kwa damu! Mimi ni katika nyinyi nanyi ni katika mimi, nitapigana na mnayepigana nae na nitampa amani mtakayempa amani.”

Ka’ab akasema: Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshkie akasema:

“Nipeni miongoni mwenu wadhamini kumi na mbili ili wawe wachunga/wakubwa wa jamaa zao.”

Wakampa watu hao kumi na mbili, tisa kutoka katika kabila la Khazraji na atatu kutoka Ausi. Mtume akawaambia wale wadhamini/wakubwa:

 “Nyinyi ndio wakubwa wa jamaa zenu, kama walivyokuwa wafuasi wa Issa Ibn Maryam, nami ni mkubwa kwa jamaa/watu wangu.” wakasema:

Naam. Wakasema: Kunjua mkono wako, Mtume akaukunjua nao wakampa ahadi ya utiifu. Kisha Mtume akawaambia: “Rejeeni makambini mwenu”.

 Akaendela kusema: Tukararejea makambini mwetu na kulala mpaka asubuhi. Kulipokucha wakatujia viongozi wa Makurayshi, wakatuambia:

“Enyi jamaa Makhazraji, imetufikia khabari kwamba nyinyi mmemjia mwenzetu huyu {Muhammad} mumchukue na mmempa ahadi ya utii kupigana nasi. Wallah! sisi tunachukia kupigana nanyi. Akaendela kusema: Wakainuka jamaa zetu mushrikina wakaapa na kusema hakuna jambo kama hilo na wala hatulijui! Akasema: Wakasadiki {Makurayshi} kwa jinsi wanavyotujua, nasi tukawa tunaangaliana wenyewe kwa wenyewe”.

Haya ndiyo maagano ya pili ya “Aqabah” yaliyotokea katika mwaka wa kumi na tatu wa utume. Maagano haya yalikuwa na taathira kubwa katika historia nzima ya da’awah ya Kiislamu.

 Maagano haya baina ya Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie na maanswari Allah awawiye radhi yalitia matumaini mioyoni mwa waislamu wanyonge waliokuwa wakiteswa na kuadhibiwa Makkah kwa sababu tu ya kumkubali Mwenyezi Mungu mmoja asiye na mshirika, tusome:

“NAO HAWAJAONA BAYA LOLOTE KWAO (Waislamu) ILA KUMUAMINI ALLAH MSHINDI (na) MWENYE KUSIFIWA. “[85:8] wakawa na yakini kwamba nusura ya Mwenyezi Mungu i karibu.

Maagano haya yakawa ni faraja kwa upande wa waislamu na pigo kubwa upande wa Makurayshi.

Maagano haya yalikuwa ni tukio lisilotazamiwa kabisa na makurayshi, kwani wao waliamini kwamba wamshamdhibiti kabisa Bwana Mtume.

Waliweka mikakati kuhakikisha kuwa da’awah ya Mtume haivuki majabali ya Makkah na kutoka nje ili isije ikawaathiri Waarabu wengine na Mtume akapata nguvu.

 Walipotambua kwamba Ausi na Khazraji, wenyeji wa Madinah wamemfuata Mtume na wamempa ahadi ya utii juu ya kumnusuru na kumlinda dhidi ya wapinzani wake, habari hii ilizigonga nyoyo zao na kuwatetemesha, akili ikawatoka.

Wakaanza kuwatafuta Maansari na kuwasihi wayavunje maagano haya ambayo ni hatari machini mwao, lakini wapi, hayawi hayawi hayo wayatakayo:

“HAKI IKASIMAMA NA YAKAHARIBIKA WALIYOKUWA WAKIYATENDA KWA HIVYO WALISHINDWA HAPO NA WAKAWA WENYE KUDHALILIKA.” [7:118-119]

Kadhalika maagano haya yakawa ni mpaka wa upambanuzi baina ya vipindi viwili vya da’awah kipindi cha majaribio na mtihani, hiki ndicho kilichokuwa kipindi cha kwanza, kipindi walichokipitia waislamu Makkah.

Kipndi cha uchache, unyonge na adhabu na mateso yasiyovumilika ila na mtu mwenye imani ya kweli na yakini thabiti.

Haya yote yalikuwa ni maandalizi ya kuwaandaa kuwa mfano wa kupigwa juu ya imani ya kweli ambayo Mwenyezi Mungu aliwataka waineze katika ardhi. Walipofaulu mtihani huu na kuonekana ukweli na nguvu ya imani yao ndipo kikaja kipindi cha malipo na jazaa ya subira na uvumilivu, Mwenyezi Mungu akawaokoa na adhabu hii.

Akawaandalia mji wa Madinah wahamie huko, na akawapa hawa ndugu wakweli (Maanswari), waliowapa makazi na wakawanusuru.

Wakagawana nao mali na majumba yao na wakawapendelea zaidi kuliko wao wenyewe. Mwenyezi Mungu akawafungulia milango ya rehema zake na akaibadilisha khofu yao kuwa amani, udhalili wao kuwa utukufu.

Mwenyezi Mungu mtukufu akawaneemesha kwa neema hizi, kuhusiana na hili tunasoma:

“ NA KUMBUKENI (Enyi waislamu) MLIPOKUWA WACHACE, MKIONEKANA MADHAIFU (Wanyonge) KATIKA ARDHI, MKAWA MNAOGOPA WATU WASIKUNYAKUENI, AKAKUPENI MAHALA  PAZURI PA KUKAA (napo ni hapa Madinah) NA AKAKUTIENI NGUVU KWA NUSURA YAKE NA AKAKUPENI RIZIKI NZURI ILI MPATE KUSHUKURU.” [8:26]

MAAGANO YA PILI YA AQABAH

Msimu uliofuatia wa Hijjah, Uislamu ulikuwa tayari umeenea kwa kiasi kikubwa katika mji wa Yahrib (Madinah).

Katika kundi kubwa la Mahujaji kutoka Yathrib lililowajumuisha pamoja waislamu na mushrikina, walikuwemo waislamu sabini na tatu, miongoni mwao wakiwemo wanawake wawili. Mtume Rehema na Amani zimshukie akapanga kukutana na ujumbe huu kutoka Yathrib “Aqabah” usiku.

Akawaagiza kutokufanya harakati zozote zitakazowafanya mushrikina waliokuja nao kuhisi kitu. wasije kama kundi, bali mtu mmoja mmoja au wawili wawili na waje baada ya kupita theluthi ya kwanza ya usiku yaani baada ya saa nne usiku na kwamba wasimsubiri asiyepo na wala wasimuashe aliyelala.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *