FIDIA YA ABUL-AASWI

Miongoni mwa mateka alikuwemo Abul-Aaaswi Ibn Rabee, huyu alikuwa ni mkwewe Mtume kwa bintie Zaynabu. Ibn Is-haaq-Allah amrehemu–anasema:

“Abul-Aaswi alikuwa ni miongoni mwa watu wa Makah walio wachache wa mali, amana na biashara.

Watu wa Makah walipowatuma watu kwenda kuwakomboa ndugu zao kwa kutoa fidia Zaynabu Binti ya Mtume wa Allah nae alimpa mtu mali kwenda kumfidia Abul-Aaswi Ibn Rabee (mumewe).

Katika mali hiyo aliyotoa kilikuwemo kidani chake alichopewa na Bi. Khadijah mama yake (mkewe Mtume) siku ya harusi yake.

Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie– alipokiona kidani cha mkewe yalimjia makiwa na huruma akasema:

“Mkiweza kumuacha huru mateka wake na kumrudushia mali yake, basi fanyeni hivyo.” Mashwahaba wakasema:

“Naam, ewe Mtume wa Allah wakumuachia na kumrudishia mali yake. Nae Mtume akachukua ahadi kwa Abul-Aaswi ya kwamba amuachie (amruhusu) Zaynabu kuhamia Madinah Abdul-Aaswi akaahidi kulitekeleza hilo”.

 

KUFIDIWA KWA ABBAAS.

Abbas Ibn Abdul-Mutwalib-Ami yake Mtume, nae alikuwa ni miongoni mwa mateka wa vita vya Badri.

Huyu alitumai kupata ihsani ya Mtume, aachiwe huru bila ya kutoa fidia. Lakini mambo hayakuwa kama alivyodhania, Bwana Mtume hakukubali kumuachia ila kwa kujitolea fidia yeye mwenyewe pamoja na jamaa nao. Zuhriy–Allah amrehemu–amepokea kwamba:

“Makurayshi waliwatuma watu kwa Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie kwenda kuwatolea fidia mateka wao. Watu wote wakawafidia mateka wao kwa namna walivyokubaliana.” Abbas akasema:

 “Ewe Mtume wa Allah, kwa yakini tayari nilishakuwa muislamu”.

Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie–akamwambia:

“Allah ndiye mwenye kujua zaidi uislamu wako (kusilimu kwako), ukiwa kama usemavyo basi hakika Allah atakujazi (atakulipa). Na lililo juu yetu sisi ni dhahiri yako ilivyokuwa, kwa hivyo jifidie nafsi yako na wana wa nduguyo; Naufal Ibn Al-Haarith Ibn Abdul– Mutwalib na Uqayl Ibn Abuu Twaalib Ibn Abdul–Mutwalib. Na umtolee fidia mshirika wako Utbah Ibn Amrou ndugu wa Banil-Haarith Ibn Fihr”. Akasema (Abbas):

“Mimi nina mali gani ya kutoa fidia, ewe Mtume wa Allah?” (Mtume) akamwambia:

“I wapi ile mali uliyoizika wewe na Ummul-Fadhli? Wewe ulimwambia (mkeo): Nikiuwawa katika safari yangu hii, basi mali hii niliyoizika ni ya wanangu; Al-Fadhli, Abdullah na Quthm.”

Akasema (Abbas):

“Wallah, ewe Mtume wa Allah, hakika kwa yakini natambua kwamaba wewe ni Mtume wa Allah! Hakika jambo hili halijui ye yote ila mimi na (mke wangu) Ummul–Fadhli (tu). Nakuomba ewe Mtume wa Allah, unifikirie katika mali mliyoiteka kwangu, nipeni wakia (ounce) ishirini kutoka katika mali niliyokuwa nayo.”

Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-akasema:

“Hapana, hicho ni kitu alichotupa Allah kutoka kwako.” Hatimaye Abbas akajifidia yeye mwenyewe, wana wa nduguye ma mshirika wake.”

 

SURA YA VITA ILITOA VIGEZO VYA USHINDI NA VIGEZO VYA USHINDWA

Tumeona waislamu wakiibuka washindi katika vita vya Badri pamoja na uchache wao, maandalizi dhaifu na zana duni ukilinganisha na mahasimu wao.

Kadhalika tumeona Makurayshi waliokuwa wengi, wenye maandalizi ya kutosha na zana nyingi na imara za vita, wakiendeshwa mbio na kushindwa vibaya sana.

Wewe mpenzi msomaji wetu, unafikiri nini zilikuwa sababu za ushindi na ushindwa huu pamoja na tofauti kubwa na ya wazi iliyokuwepo baina ya makundi mawili haya; kundi dhaifu na kundi lenye nguvu?

Nini ilikuwa siri ya ushindi wa kundi hili dogo tena dhaifu dhidi ya kundi kubwa lenye nguvu na maandalizi ya kutosha?

Ushindi uliowashangaza si tu washindwa bali hata washindi pia.

Ushindi unaovibatilisha vigezo vya ushindi kama vilivyokuwa katika fira za watu, na natija ya vita kuwa kinyume na mazoea ya watu.

Hapana shaka yo yote kwamba ushindi huu wa kishindo wa waislamu, ulitokana na msaada wa Allah. Allah aliwasaidia waumini kwa nguvu zake zisizoshindika, akawateremshia majeshi ya malaika kuwasaidia bila ya wao kuyaona:

“….NA AKATEREMSHA MAJESHI (ya malaika) AMBAYO HAMKUYAONA NA AKAWAADHIBU WALE WALIOKUFURU NA HAYO NDIYO MALIPO YA MAKAFIRI.” (9:26)

Allah akawaandikia waumini ushindi ikiwa ni jazaa ya subira na ukweli wao pamoja na ustahamilivu waliouonyesha katika machungu yote yaliyowafika kwa ajili ya dini ya Allah.

Na kujitoa kwao muhanga kuinusuru dini ya Allah na Mtume wake na kusimama kwao kidete katika kuilinda Imani yao.

Ukiziachilia mbali sababu hizi, bila ya shaka kwa mchunguzi na mzingatiaji wa mambo atagundua sababu nyingine za ziada. Sababu ambazo zinaweza kuonekana machoni kuwa ndogo lakini kwa hakika zilitoa mchango mkubwa katika kufikia ushindi. Tunaweza kuzielezea sababu hizo kama ifuatavyo:

 

WAISLAMU WALIPIGANA KWA NIA NA SHAURI MOJA

Waislamu walitoka Madinah kuelekea Badri wakiwa na nia na shauri moja chini ya kiongozi mmoja.

Wakiwa na lengo moja tu nalo si jingine bali ni kuuteka msafara wa biashara wa makurayshi. Walipobaini kwamba msafara umewaponyoka na kwamba Makurayshi wamewatokea kuja kuwasagasaga.

Msimamo wao ukabadilika na udhaifu ukazipenya safu zao, kiongozi na kamanda wao Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie–akalidiriki hili.

Akawarejesha katika nguvu na ari na akawakusanya pamoja juu ya nia moja kiasi cha kutoweza kujitoa katika jamaa mtu ye yote.

Wakateremka katika uwanja wa mapambano wakiwa wamejawa mori na ari ya haki ambayo wanayoipigania na kuitetea.

Na lengo lao wakati huo lilikuwa ni moja tu, nalo ni dini ya haki kuzishinda dini zote potofu, na neno la Allah kuwa juu ya kila neno.

Wakajitoa muhanga katika kulitimiza lengo hili na waumini wakayasahau kabisa mapambo (starehe) ya maisha ya dunia. Kila mmoja akawa hawanii na wala hapanii ila kufa shahidi kwa ajili ya dini ya Allah.

 

B) MAKAFIRI WALIPIGANA NA IL-HALI NYOYO ZAO ZIMETAPANYIKA (HAWAKO PAMOJA)

Mushrikana kwa upande wao, walitoka wakiwa wamechangukana hawaunganishwi na uongozi mmoja. Wala haiwakusanyi pamoja nia na lengo moja.

Lilikuwepo kundi miongoni mwao lililokuwa na lengo la kulipa kisasi kwa Muhammad; Mtume wa Allah–na maswahaba wake na kundi lingine halikutoka ila kwa lengo la kuhami na kuuokoa msafara wao wa biashara.

Hawa zilipowafikia khabari za kunusurika kwa msafara wao wakagawika makundi mawili. Kundi moja likaona hakuna tena mantiki ya vita likajitoa na kuamua kurejea Makah na kundi jingine pamoja na kutoona sababu ya vita lakini likalazimika kuwemo kundini kwa kuona vibaya kujitenga na wenzao.

Haya yalikuwa kabla ya kuanza kwa mapambano. Mkundi mawili yalipokutana katika uwanja wa mapambano, makafiri wakaona nyusoni mwa waislamu utayarifu wa kujitolea muhanga, ukadhihiri mgawanyiko kwa mara nyingine tena.

Baadhi ya wakubwa wao wakaanza kuwahamasisha kuingia vitani. Yakakhitilafiana makundi mawili haya kiasi cha kuzozana viongozi wao na kuwafanya waingie vitani wakiwa na chuki wao kwa wao na nyoyo zilizogawika.

Kadhalika lilikuwemo mapambanoni kundi ambalo halikudhamiria uadui na mfundo si kwa Mtume wala kwa waumini. Hili lilikuwa ni kundi la Baniy Haashim na washirika wao.

Hawa kidhahiri walikuwa pamoja na mushriki, lakini nyoyo zao zilikuwa pamoja na waislamu. Ni kwa sababu hii ndio Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie–akawausia maswahaba wake wasimuue ye yote miongoni mwa watu wa kundi hili.

Kwa hali hii utawaona mushrikina wameingia katika uwanja wa mapambano wakiwa si wamoja; nyoyo zao zimetengana na malengo tofauti.

Uongozi wao ukiwa umeparaganyika, hawana kiongozi mmoja mwenye kutiiwa na kukubalika na wote. Wakati ambapo waislamu walipambana nao wakiwa na lengo moja, moyo mmoja chini ya kiongozi mmoja.

 

FIDIA YA ABUL-AASWI

Miongoni mwa mateka alikuwemo Abul-Aaaswi Ibn Rabee, huyu alikuwa ni mkwewe Mtume kwa bintie Zaynabu. Ibn Is-haaq-Allah amrehemu–anasema:

“Abul-Aaswi alikuwa ni miongoni mwa watu wa Makah walio wachache wa mali, amana na biashara.

Watu wa Makah walipowatuma watu kwenda kuwakomboa ndugu zao kwa kutoa fidia Zaynabu Binti ya Mtume wa Allah nae alimpa mtu mali kwenda kumfidia Abul-Aaswi Ibn Rabee (mumewe).

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *