IQMA

Iqaamah kama ilivyo adhana ni suna muakadah (kokotezwa) katika swala za fardhi zinazoswaliwa ndani ya wakati wake (Adaa) au zinazoswaliwa nje ya wakati wake (Qadhwaa).

Iqaamah ni suna kwa jamaa na mwenye kuswali pekee kwa watu wanamume na wanawake.

Iqaamah ni mithili ya adhana ila kwa tofauti chache zifuatazo:-

Matamko ya adhana ni mara mbili mbili wakati ambapo matamko ya Iqaamah ni mara moja moja tu. Dalili juu ya hili ni hadithi ya Anas-Allah amuwiye radhi:

“Bilali aliamrishwa kuifanya shaf-i adhana na kuiwitirisha iqaamah, ila tamko la iqaamah (Qad Qaamatis-swalaah)”. Bukhaariy & Muslim

Shaf-i ni hesabu iwezayo kugawika kwa mbili, na witri ni ile isiyogawika kwa mbili.

IQAMA NA TAMKO LAKE

Iqaamah kama ilivyo adhana ni suna muakadah (kokotezwa) katika swala za fardhi zinazoswaliwa ndani ya wakati wake (Adaa) au zinazoswaliwa nje ya wakati wake (Qadhwaa).

Iqaamah ni suna kwa jamaa na mwenye kuswali pekee kwa watu wanamume na wanawake.

Iqaamah ni mithili ya adhana ila kwa tofauti chache zifuatazo:-

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *