MILA ZINAZOKHALIFIANA NA SHERIA

Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia ndani ya Qur-ani Tukufu:

 

“ENYI MLIOAMINI !INGIENI KATIKA HUKUMU ZA UISLAMU ZOTE, WALA MSIFUATE NYAYO ZA SHETANI, KWA HAKIKA YEYE KWENU NI ADUI DHAHIRI”.

Hili nitangazo na agizo la Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila ambaye ameukiri na kuukubali uislamu kwa khiyari yake mwenyewe.

Katika tangazo na amri hii analazimishwa kila muislamu kuufuata uislamu mzima kama mfumo wa maisha yake yote.

Aufuate uislamu katika maisha yake ya kijamii, kiuchumi,kielimu, kiulinzi, kiibada na baki nyanja nyingine za maisha yake.

Atambue kuwa uislam kama dini ndio mfumo sahihi wa sheria, mila na utamaduni umfaao mwanadamu. Ni mfumo ulio kamilika, kwa mantiki hii uislamu,uislamu hauna upungufu na wala hauhitajii ziada yoyote kutoka popote pale. Haya yanathibitishwa na kauli tukufu ya Mola Mtukufu:

“LEO NIMEKUKAMILISHIENI DINI YENU, NA KUKUTIMIZIENI NEEMA YANGU, NA NIMEKUPENDELEENI UISLAMU UWE DINI YENU….”[5:3]

Aya inaeleza bayana kuwa uislamu ndio mfumo sahihi na kamili wa maisha, uislamu ni Neema ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu kwa waja wake uislamu ndio dini TEULE na CHAGUO la Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake.

Kwa mantiki hii, leo waislamu kuhukumiana nje ya Qur-ani , kufuata mila na tamaduni zinazokhalifiana na sheria ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu ni sawa na kuibatilisha aya hiyo hapo juu isemayo kuwa uislamu umekamilika.

Matendo yao hayo yanaonyesha kuwa uislamu umesahau kuyawekea sheria, kanuni na taratibu baadhi ya maeneo katika maisha ya mwanadamu.

Kwa hivyo, wao wanayo fursa ya kujipangia sheria, kanuni na taratibu zitakazokidhi haja zao katika maeneo husika bila kujali wala kuangalia kuwa kanuni na taratibu hizo zinapingana na sheria ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu na isitoshe bado watu hawa waliojiundia mila na tamaduni zao nje ya uislamu bado wanadai na kujiita kuwa ni waislamu. Mtu ana khiyari ya ama kuwa au kutokuwa muislam, kwa ushahidi wa kauli yake Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu :

“HAKUNA KULAZIMISHWA (mtu kuingia)KATIKA DINI UONGOFU UMEKWISHA PAMBANUKA NA UPOTEFU BASI ANAYEMKATAA SHETANI NA AKAMWAMINI ALLAH BILA SHAKA YEYE AMESHIKA KISHIKO CHENYE NGUVU KISICHOKUWA NA KUVUNJIKA…”[2:256]

Na akasema tena :

“NA SEMA : “HUU NI UKWELI ULOTOKA KWA MOLA WENU BASI ANAYETAKA NAAMINI NA ANAYETAKA NA AKUFURU ….”[18:29]

Mtu akishautumia uhuru na khiyari aliyopewa na akauchagua uislamu kama dini na mfumo wa kuyatawala maisha yake yote, hapo sasa hana khiyari tena ya kuchagua hukumu/sheria zipi za uislamu asifuate na zipi asizifuate, bali analazimishwa kuzifuata shria zote.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anaikemea vikali tabia hii ya kufuata baadhi ya hukumu/sheria na kuacha nyingine, tusome na kutafakari :

“… JE! MNAAMINI BAADHI YA KITABU NA KUKATAA BAADHI (yake) ? BASI HAKUNA MALIPO KWA MWENYE KUFANYA HAYA KATIKA NYINYI ILA FEDHEHA KATIKA MAISHA YA DUNIA ; NA SIKU YA KIYAMA WATAPELEKWA KATIKA ADHABU KALI ….”[2:85]

Mwenyezi Mungu Mtukufu anazidi kutuambia na kutuonyesha kuwa Muislamu wa kweli hana khiyari, uhuru wala uchaguzi katika kufuata ama kutokufuata sheria/hukumu za kiislamu kama mfumo sahihi wa maisha, tusome na tuzingatie:

“HAIWI KWA MWANAUME ALIYEAMINI WALA KWA MWANAMKE ALIYEAMINI, ALLAH NA MTUME WAKE WANAPOKATA SHAURI, WAWE NA HIARI KATIKA SHAURI LAO, NA MWENYE KUMUASI ALLAH NA MTUME WAKE, HAKIKA AMEPOTEA UPOTOFU ULIO WAZI(kabisa)”. [33:36]

Mpaka hapa, tayari tume kwisha thibitisha kuwa uislamu ni dini iliyokamilika na kwamba mwislamu hana uchaguzi katika kufuata ama kutokufuata hukumu/sheria za uislamu.

Muislamu hana fursa hata kidogo ya kujiundia kanuni, taratibu, mila au desturi na ada zilizo nje ya uislamu, kitendo hicho ni kosa kubwa ambalo limeandaliwa adhabu kali iumizayo na kutia uchungu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Hebu sasa tujaribu kuziangalia baadhi ya mila, tamaduni, desturi na ada zinazokhalifina na kupingana na sheria.

Desturi na ada hizi tunazoishi nazo kataka jamii na kurithishana kizazi hata kizazi zimezoeleka na kuota mizizi katika jamii zetu kiasi cha kusifanya zionekane kuwa ni za kawaida na zinakubalika katika dini, na ukweli ni kwamba hazina nafasi kabisa katika dini hii iloyokamilika na kujitosheleza

 

MILA ZINAZOKHALIFIANA NA SHERIA

Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia ndani ya Qur-ani Tukufu:

 

“ENYI MLIOAMINI !INGIENI KATIKA HUKUMU ZA UISLAMU ZOTE, WALA MSIFUATE NYAYO ZA SHETANI, KWA HAKIKA YEYE KWENU NI ADUI DHAHIRI”.

Hili nitangazo na agizo la Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila ambaye ameukiri na kuukubali uislamu kwa khiyari yake mwenyewe.

Katika tangazo na amri hii analazimishwa kila muislamu kuufuata uislamu mzima kama mfumo wa maisha yake yote.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *