SWALI LA WIKI (JUMA LA 78)

SWALI: Ni jambo lililo tangaa na limekuwa kama ada katika jamii zetu, mwanamume kunyonya chuchu/maziwa ya mke wake. Naomba kufahamishwa hukumu ya sharia katika jambo hilo.

JIBU: Mume kunyonya chuchu za mke wake si jambo la haramu bali ni katika jumla ya zile aina/sampuli za kustarehe baina ya mke na mume kuliko ruhusiwa na sharia. Sharia imewaruhusu wanandoa kuchezeana viungo vyote vya mwili vitakavyo amsha hamu na kuwaletea nyege ya kufanya tendo la ndoa baina yao. Ila tu isiwe katika tupu ya nyuma.

Na katika kipindi cha kunyonyesha mume hatakiwi kunyonya maziwa ya mkewe kiasi cha kufikia kumpunja mwanawe mdogo chakula chake hicho.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *