AKHLAAQ NI NINI?
Elimu ya akhlaaq ni elimu ya malezi ya tabia ambayo hujihusisha na kutengenea kwa moyo kwa kuupamba na tabia njema na kuuepusha na tabia mbaya.
Elimu hii msingi wake ni Qur-ani Tukufu na Hadithi. Amesema Mwenyezi Mungu katika kusifia Mtume wake juu ya tabia njema:
“NA BILA SHAKA UNA TABIA NJEMA KABISA“(68:4) Bwana Mtume naye anaukiri na kuuthibitisha ukweli huu pale aliposema:
“Hakika si vingine nimetumwa kuja kutimiza TABIA NJEMA” Al-Bukhaariy
FAIDA ZA ELIMU YA AKHLAAQ:
Elimu hii husaidia kuutengeneza moyo wa mwanadamu ikamtoa katika unyama, ikamfinyanga na kumfanya kuwa mtu mwema, aliyepambika na sifa na tabia njema na kumuepusha na tabia mbaya, na ikawa ndiyo sababu ya kufaulu duniani na akhera.
“Aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu juu ya mambo yanayoingiza watu peponi kwa wingi,akasema: (Kumcha Mungu na tabia njema)” At-twabraaniy
Elimu hii pia humsaidia mtu kuzijua tabia njema akazifuate na tabia mbaya akaziepuka.