UPENDO

Hebu sasa tuingalie swala ni kwa kiasi gani inaweza kuwa ni kiwanda kinachozalisha bidhaa adimu na muhimu “Upendo”.

Hebu itazameni swala wakati waislamu wanapokusanyika mahala pamoja mbele ya Bwana Mlezi wa viumbe wote, sio Bwana wa uma mmoja, Taifa moja wala dini/mfumo mmoja wa maisha bali ni Bwana Mlezi wa viumbe wote Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.

Ambaye huwabubujishia na kuwamiminia rehema yake woote, waislamu na wasio waislamu (makafiri) watiifu na waasi, wema na waovu, wadogo na wakubwa kisha angalia namna muislamu anavyoikhitimisha swala yake kwa kusema, Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah! Hapa anawakumbuka ndugu zake waliotapakaa mashariki na magharibi ya ardhi.

Kisha anatoka ndani ya swala kwa REHEMA na AMANI, husema Amani na Rehema ya Allah iwe juu yenu.

 Aliianza swala yake kwa tuamko la “ALLAAHU AKBAR!”

Allah ni Mkubwa kuliko wakubwa wote, na sasa anaikhitimisha kwa tamko la Amani na Rehema.

Haya yote ni vigezo na vielelezo tosha kwamba nguvu ya Uislamu ni nguvu inayokomelea na Rehama na Amani vitu ambavyo ndio chemchem ya upendo.

Hivi ndivyo swala inavyoweza kupandikiza nguvu ya upendo na moyo wa kuzoeana na kupendana baina ya waislamu khasa khasa katika swala za jamaa,

FALSAFA YA SWALA: 2.UPENDO

Hebu sasa tuingalie swala ni kwa kiasi gani inaweza kuwa ni kiwanda kinachozalisha bidhaa adimu na muhimu “Upendo”.

Hebu itazameni swala wakati waislamu wanapokusanyika mahala pamoja mbele ya Bwana Mlezi wa viumbe wote, sio Bwana wa uma mmoja, Taifa moja wala dini/mfumo mmoja wa maisha bali ni Bwana Mlezi wa viumbe wote Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *