UISLAMU

Uislamu ndio dini ya maumbile bila ya makindano.

Yaani Uislamu ndio mfumo wa maisha unaokwenda sambamba na maumbile ya mwanadamu na ulimwengu wake.

Kwa mantiki hii tunaweza kusema kwa kinywa kipana kabisa kwamba Uislamu ndio dini ya jamii ya wanadamu.

Uislamu haukuitwa dini ya jamii ya wanadamu kwa kuropoka tu au kwa hamasa na jazba. Imeitwa hivyo kwa sababu zifuatazo:-

1. Imesheheni desturi zinazokubaliana na akili.

2. Ina uongofu unaouangazia na kuupa nuru moyo.

3. Inabeba maendeleo yanayofaa kwa hali, mahala na zama zote.

4. Ina sheria inayokidhi hali na mahitaji yote ya jamii katika nyanja zote za maisha.

5. Ina dhana ya usawa unaowaunganisha pamoja watu wote bila ya kujali lugha, rangi au hali zao za kimaisha.

6. Sheria yake ina dhima ya kumpa mwanadamu maisha ya amani, utulivu, raha, furaha na heshima katika nafsi, mwili, akili na mali.

Haya na mengineyo ndiyo yanayoufanya Uislamu uwe ni dini inayokubaliwa na kuridhiwa na mwanadamu kwa kuwa inayogusa moja kwa moja maumbile yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *