Ni wajibu kwa mwenye kuswali akae baada ya sijda ya mwisho ya swala yake asome “Tashahudi” imepokelewa katika riwaya ya Ibn Masoud Allah amuwiye radhi – amesema : Tulikuwa tukisema kabla ya kufaradhishwa juu yetu Tashahudi
ASSALAAM ALALLAH KABLA IBADIHI, ASSALAAM ALAA JIBRILL, ASSALAAM ALA MIIKAIL, ASSALAAM ALA FULAN
Mtume – Rehema na amani zimshukie alipomalizaa kuswali alituelekkea , akatuambia “ Hakika Allah ndiye AS – SALAAM , basi anapokaa mmoja wenu katika swala { Kwa ajili ya Tashahudi } basi na aseme
ATTAHIYYAAT LILLAH WASSALAWATU WATTAYYIBAATU, ASSALAAM ALAYKA AYYUHA NNABII WARAHMATULLAH WABARAKATUH, ASSALAAM ALAYNA WA-ALAIBADILLAHI SSALIHINA
Kwani nyinyi mtakapoisema {salamu hii} humpata {humfikia} kila mja mwema mbinguni na ardhini. Bukhaari na Muslim.
Hili ni mojawapo ya matamko sahihi ya Tashahudi ambayo yaliyonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume. Tashahudi yeyote iliyothibiti kutoka kwa Mtume mtu akiisoma itamjuzia.
Sharti za Tashahudi.
Msomaji wa Tashahudi analazimika kuchunga yafuatayo:
1. Ajisikizishe yeye mwenyewe matamko ya Tashahudi iwapo hana tatizo la kusikia.
2. Kukifululiza kisomo cha tashahudi, yaani asiweke mwanya mkubwa baina ya ibara za Tashahudi . pia asitie kati dhikri nyingine , akifanya hivyo yaani akinyamaza kinyamao kirefu au akilia kati dhikhri nyingine , Tashhahudi yake itakuwaa imebatilika na itamuwajibikia kuianza upya.
3. Aisome katika hali ya kukaa isipokuwa katika mazingira ya dharura tu ndio anaruhusiwa kuisoma katika hali yoyote imkinikiayo.
4. Aisome kwa lugha ya Kiarabu . Akishindwa atasoma tafsiri yake kwa Lugha yake, Lakini bado atakuwa na wajibu wakujifunza mpaka aweze kuisoma kiarabu kama alivyofanya Mtume wa Allah- Rehema na Amani zimfikie.
5. Achunge matokeo ya herufi , shada na hukumu zote za usomaji . akifanya kosa lolote litakalopelekea kuharibika kwa maana, halitamaanisha zaidi ya kubahatilika Tashahudi yake hiyo . Kwa hivyo basi itamlazimu kuirejea upya .
6. Ayatungamanishhe maneno ya Tashahudi kwa mtungo wake kama yalivyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie .