TAKBIRA YA KUHIRIMIA

Takbira ya kuhirimia ya swala ndio nguzo ya tatu ya swala, hii ni kusema wakati wa kuingia ndani ya swala  ALLAAHU AKBAR.

Hili linatokana na tendo lake mwenyewe Bwana Mtume na ni yeye  ndiye aliyetuagiza: “Swalini kama mlivyoniona nikiswali”. Bukhaariy.

Takbira ya kuhirimia katika suna

1. Imepokelewa na Sayyidna Abdullah Ibn Umar-Allah amuwiye radhi – amesema:

“ Alikuwa Mtume wa Allah- Rehema na Amani zimshukie- anaposimama kwa ajili ya kuswali, hunyanyua mikono yake mpaka ikawa mkabala wa mabega yake kisha akasema ALLAHU AKBAR………” Muslim.

2.   Imepokelewa na Sayyidna Abu Hurayrah-Allah amuwiye radhi-amesema:

    “Alikuwa Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – anaposimama kwenye swala kusema ALLAAHU AKBAR wakati anaposimama……..” Muslim.

3.   Imepokelewa na Imam Aliy – Allah amuwiye radhi amesema: Amesema  Mtume wa Allah – Rehma na Amni zimshukie:  

     Ufunguo wa swala ni udhu, na kiharamisha chake (swala) ni takbiria na kihalalisha chake ni salamu” Turmidhiy na Ibn Maajah

Mwenye kuswali atakapohirimia swala kwa kusema ALLAAHU AKBAR, inamuharamikia kusema kauli au kutenda tendo lililo nje ya matendo au kauli zinazoijenga swala mpaka atakapotoa salamu. Kwa hivyo utaona kuwa Takbira ya kuhirimia ndio ufunguo wa kuifungulia swala na salamu inaashiria mwisho wa swala.

Tamko la Takbira

Tamko la Takbira ya kuhirimia swala kama lilivyopokelewa kutoka kwa Bwana Mtume ni ALLAAHU AKBAR.

Mtume hakuwahi kuifungua swala kwa kutumia tamko lingine zaidi ya hili na kumfuata yeye ni wajibu kwetu sisi.

Sharti za Takbiria ya kuhirimia.

Ili Takbiri isihi, kumeshurutizwa kuchunga mambo yafuatayo

 

i.  Mwenye kuswali alitamke tamko la Takbira akiwa amesimama wima na hatembei.

Hili linatokana na maelekezo ya Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alipomwambia yule swahaba aliyemuona haswali itakiwanvyo, akamwambia:

“Unaposimama kwenye swala leta Takbiriia (sema ALLAAHU AKBAR)” Bukhaariy na Muslim.  

Katika hadithi hii Bwana Mtume anamshrutizia swahaba huyu kuhirimia akiwa amesimama.

ii.     Alitamke akiwa ameelekea Qiblah.

iii.     Tamko la Takbira litamkwe kwa lugha ya Kiarabu.

Hili lni kwa mujibu wa agizo lililotolewa na Mtume – Rehema na Amani zimshukie:”

Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali”.

Haikupokelewa riwaya yeyote kwamba Mtume alilitamka tamko hili la Takbira kwa lugha isiyo ya kiarabu, kwa hivyo ikatuwajibika nasi tulitamka kama alivyolitamka mwalimu wetu huyu.

Mas-ala: Inamuwajibikia mtu asiyejua kiarabu ajifunze mpaka aweze kulitamka tamko la Takbira ya kuhirimia kwa kiarabu.

Kadhalika inamlazimu ajifunze kutamka dhikri zote za wajibu katika swala kwa kiarabu. Fahamu na uelewe, akishindwa kabisa, basi inamjuzia kuzitamka hizo dhikri kwa lugha yake aiwezayo ila Qur-ani tu ndio haitamkwi ndani ya swla ila kwa Kiarabu pekee.

Mahala pa kusoma Qur-ani katika swala anaweza kuleta dhikri nyingine kama tasbiyh, tahmiyd, tahliyl na takbiyr. Hivi ndivyo tunavyoelekezwa na Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie.

Imepokelewa na Ibn abiy Awfaa-kwamba mtu mmoja alisema, Ewe Mtume wa Allah, nifundishe kitu kitakachonitosheleza na Qur-ani (Mtume) akamwambia:

“Sema: sub-haanallah (Tasbiyh), Wal-hamduli llaah (Tahmiyd) wa laa Illaha illal – laah (Tahilyl) wallaahu akbar (Takbiyr)” Ibn Hibbaan.

 

(iv)    Tamko hili likutanishwe na nia, yaani usiwepo mwanya baina ya nia na Takbira hii ya kuhirimia swala.

 

TAKBIRA YA KUHIRIMIA

Takbira ya kuhirimia ya swala ndio nguzo ya tatu ya swala, hii ni kusema wakati wa kuingia ndani ya swala  ALLAAHU AKBAR.

Hili linatokana na tendo lake mwenyewe Bwana Mtume na ni yeye  ndiye aliyetuagiza: “Swalini kama mlivyoniona nikiswali”. Bukhaariy.

Takbira ya kuhirimia katika suna

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *