SWALI: Mwanamke mtaabadi, anapenda Swakuswali jamaa msikitini khususan swala ya Tarawehe ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nini mtazamo na hukumu ya sheria katika kadhia hii ya mwanamke kwenda msikitini usiku?
JIBU: Hakuna kinacho mzuia mwanamke kwenda kuswali swala ya Tarawehe au nyenginezo msikitini katika jamaa, ikiwa atachunga sharti hizi:
- Atoke akiwa amevaa kama atakiwavyo kuvaa na sharia.
- Kutoka kwake kusihatarishe amani na usalama wake kwa sababu yoyote ile iwayo.
- Kutoka kwake kusiwe ni sababu ya kuacha kutekeleza yale yenye umuhimu mno kwake, mithili ya ulezi wa wanawe au kumuangalia mume wake aliye mgonjwa na mambo kama hayo.
- Kupata idhini na radhi ya mume wake katika kutoka kwake huko.
Allah ndiye Mjuzi mno.