SWALI LA WIKI(JUMA LA 66)

SWALI: Zama zetu za leo, hima na adabu ya watu katika ibada imeshuka kwa kiwango kikubwa. Utamuona mtu anachati au anaongea na mwenzake huku khatibu yuko juu ya mimbari anatoa khutba ya Ijumaa. Swali, je kuzungumza wakati khatibu anakhutubu siku ya Ijumaa, kunabatilisha swala?

JIBU: Kuzungumza wakati wa khutba ni HARAMU na jambo hilo puo (mchezo), tena linapunguza au kuondosha kabisa thawabu za swala. Na ifahamike ya kwamba khutba ya Ijumaa ni sehemu ya swala ya Ijumaa, kwa sababu sisi huswali Adhuhuri rakaa nne na tunaswali Ijumaa rakaa mbili ambayo inatutoshelezea ile swala ya Adhuhuri. Ndio maana tukishaswali Ijumaa, hatuswali Adhuhuri na khutba ndio husimama mahala pa zile rakaa mbili nyingine. Ni kwa ajili/sababu hiyo basi, ndio ikawa ni WAJIBU kunyamaza; kuacha kuzungumza wakati inapo tolewa khutba.

Na makatazo ya kuacha kuzungumza wakati wa khutba yamezuia hata kumwambia nyamaza yule anaye zungumza. Na mtu akimnyamaza mwenzake naye huyo atahesabika kuwa amefanya mchezo na hata yule atakaye chezea japo jiviwe pia amecheza huyo. Mambo yote hayo yanaondosha na kupunguza thawabu na ujira wa swala ya Ijumaa mbele za Allah.

Tanbihi: Lakini si wajibu kwa aliye fanya mchezo wakati wa khutba kwa namna tuliyo itaja, swala yake ni sahihi na wajibu umeshamuondokea, lakini itakuwa na ujira kidogo au itakosa kabisa.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *