SWALI LA WIKI

SWALI: Msikitini kwetu tunaswalishwa na Imamu ambaye kwa kweli mimi binafsi siridhiki nae; sina imani nae. Je, nini hukumu ya swala yangu nyuma ya Imamu huyu, swala yangu ni sahihi?
JIBU: Maamuma atakaye swalishwa na Imamu ambaye yeye hana imani naye, swala ya huyo maamuma ni sahihi, kwani Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema katika hadithi ndefu: “…wanakuongozeni katika swala (wanakuswalisheni) wakipatia, mtapata thawabu nyinyi na wao na wakikosea, mtapata thawabu nyinyi na wao watapata dhambi”.
Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *