SWALI: Naomba kujua hukumu ya sheria katika utumiaji wa alkoholi katika masuala ya tiba; yaani kuifanya kuwa ni sehemu ya viambata vya dawa?
JIBU: Ni haramu kujitibu kwa kunywa alkoholi (pombe) ikiwa hiyo alkoholi ni katika vile ambavyo vikinywewa kwa wingi hulewesha.
Hayo ni kwa mujibu wa kauli ya swahaba Abdullah bin Masoud-Allah awawiye radhi: “Allah hakuweka tiba (ponyo/pozo la maradhi yenu) ndani ya vile mlivyo harimishiwa”.
Angalia, ikiwa mchanganyiko huo wa alkoholi umemezwa na hiyo dawa kwa kiwango cha kutokulewesha itakapo nywewa na mgonjwa. Basi hiyo itaingia chini ya uvungu wa vyenye kusamehewa na wala hakukatazwi kunywewa kama dawa.
Allah ndiye Mjuzi mno.