SWALI: Mimi ni mwanafunzi na katika mitihani yangu mara nyingi huwa nakopi majibu. Nini mtazamo wa sharia katika hilo, je hiyo ni ghushi (udanganyifu)?
JIBU: Kama kunakili katika mtihani si mojawapo ya aina za wazi kabisa za ghushi iliyo katazwa na sharia, itakuwa ni nini kingine?!
Ni dhaahiri kabisa ya kwamba jawabu la swali lako hilo halina makindano baina ya Wanazuoni wote; yeyote atakaye ulizwa swali hilo bila ya shaka jawabu lake litakuwa hiyo ni ghushi na si vinginevyo.
Kwani Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alikwisha sema: “Yeyote atakaye fanya ghushi (udanganyifu), huyo si miongoni mwetu”.
Allah ndiye Mjuzi mno.