SWALI LA WIKI (JUMA LA 85)

SWALI: Katika maisha yangu, nimetenda niliyo tenda katika maasi/madhambi; nimeacha swala, nimeiba, nimezini, nimekula riba, nime…, nime… Dhamiri yangu inanisuta na kuniuma sana na sasa ninaswali. Je, swala yangu ya unyenyekevu na ukweli, inafaa na inatosha kufuta yaliyo pita, yanayo niumiza roho na dhamiri yangu?

JIBU: Unapaswa kufahamu ya kwamba ile toba inayo maanisha kuazimia kujivua kutoka kwenye maasi na kule kujuta kwa kuyatenda, toba hiyo kwa yakini kabisa ndio kafara ya kuyafuta hayo yaliyo pita katika maasi/madhambi.

Yaani, Allah atayafuta na kukusamehe na hatakuadhibu kwa sababu ya toba ya kweli, kwani ni Yeye ndiye aliyesema: “NA HAKIKA MIMI NI MWINGI WA KUSAMEHE KWA ANAYE TUBIA NA AKAAMINI, NA AKATENDA MEMA, TENA AKAONGOKA”. Twaaha [20:82]

Na Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Aliye tubia dhambi ni kama asiye na dhambi”.

Ila tu iwapo maasi uliyo yafanya ndani yake imo haki ya watu, kama huko kuiba au kuzini na mke wa mtu. Hapo toba haitakubaliwa; haitakamilika mpaka urejeshe haki za watu kwa wastahiki wake au ukawaombe msamaha, wakusamehe ndipo utasamehewa na Allah.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *