SWALI: Mchinjaji na muuza nyama wa kitongoji/mji wetu, haswali wala hafungi Ramadhani na pamoja na hayo yeye anatenda aliyo yakataza Mola; anavaa dhahabu (pete na mkufu) na anafanya ghushi (anapunja) katika mizani. Basi je, inajuzu kula nyama inayo chinjwa na kuuzwa na mtu huyo muovu?
JIBU: Fahamu ewe muulizaji ya kwamba mtu kutokuwa muovu (aswi) si katika jumla ya sharti za kujuzu kula kichinjwa cha mchinjaji.
Na hakika si vinginevyo, sharti lililopo ni kwamba mchinjaji awe ni muislamu au mtu wa kitabu (Ahlul-Kitaab) na kitendo kizima cha uchinjaji kifuate utaratibu/mfumo ulio wekwa na sheria.
Hayo mawili yakipatikana, chinjo litasihi na kutajuzu kula nyama ya kichinjwa hicho hata kama mchinjaji ni mtu fasiki; haswali na anatenda madhambi yenye kuangamiza na kujipamba kwa dhahabu.
Allah ndiye Mjuzi mno.