SWALI LA WIKI (JUMA LA 81)

SWALI: Katika hospitali za umma, hutolewa huduma ya chakula kwa wagonjwa walio lazwa hapo. Swali, je kunajuzu mfanyakazi wa hospitali hiyo kula chakula cha wagonjwa pale kinapo bakia?

JIBU: Chakula kinacho pikwa hospitalini maalumu kwa ajili ya wagonjwa, haifai na haijuzu kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo kula hata kidogo, hata kama kitawatosheleza wagonjwa na kubakia.

Lakini chakula kikiwa kingi kuliko mahitaji ya wagonjwa na ikathibitika ya kwamba kile kilicho bakia ama kitatupwa majaani au kuachwa kiharibike.

Hapo hakuzuiliki kutafuta namna ya kukuhifadhi hicho chakula kilicho zidi/bakia, kwa kuliwa na yeyote mwenye njaa au muhitaji (masikini/fakiri na mfano wao). Lakini ni bora kupata radhi na ruhusa ya idara ya chakula au mamlaka husika za taasisi hiyo.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *