SWALI LA WIKI (JUMA LA 80)

SWALI: Mimi ni muuza uturi (manukato) na ili kumshawishi mnunuzi hulazimika kumpakaza ili apate kunusa harufu yake. Kisha tena ninakiuza kichupa cha uturi ule kwa  mtu mwingine, kikiwa tayari kimeshapungua kidogo. Naomba kujua sharia inasemaje katika hili?

JIBU: Ada/mazoea ya watu wa mahala husika ndio inachukua jukumu la kubainisha hukumu katika mas-ala hayo. Na ijulikanavyo ni kwamba chupa iliyo jaa uturi, haiathiriwi na kumpakaza mtu mmoja, wawili au watatu sehemu kidogo ya uturi uliomo ndani ya chupa hiyo.

Lakini ikiwa watapakazwa watu wengi chupa hiyo hiyo kiasi cha kuonekana upungufu wa manukato hayo kwa kutumia kipimo kile kile cha ada/mazoea ya watu. Ili bei isihi katika hali/mazingira hayo, ni wajibu kumbainishia mnunuzi, akiridhia bei imepita na imesihi.

Na kama hakuridhia, basi bei haitasihi ila kwa njia ya maridhiano, mathalan wakubaliane kupungua kwa thamani, kama alikuwa anauza kwa shilingi elfu mbili akamuuzia kwa shilingi elfu moja na mia tano, mathalan.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *