SWALI: Je, baba au kaka anayo haki ya kutumia au kula mahari ya binti au dada yake?
JIBU: Lazima ifahamike na ieleweke na wazazi na ndugu wa Bi. Harusi bali Waislamu wote ya kwamba mahari ni haki maalumu aliyopewa mke. Kwa hivyo basi, haifai na wala haijuzu kwa baba yake au ndugu yake yeyote kuchukua chochote katika mahari yake ila kwa idhini na radhi yake.
Na maneno ya Allah katika kadhia hii yako wazi na ni ya kutinda: “Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni kipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha”. An-nisaa [04]:04
Allah ndiye Mjuzi mno.