SWALI LA WIKI (JUMA LA 74)

SWALI:

Mwanaadamu hupitia hatua mbali mbali katika afya yake, kwa sababu ama ya utu uzima au maradhi imefikia hawezi kuzuia mkojo, unamtoka pasina hisia. Nini hukumu ya sheria kwa mtu huyu katika utekelezaji wa ibada zake khususan swala?

JIBU:

Katika jumla ya mambo maalumu ya dini ya Uislamu ambayo ni dini ya maumbile, ni kwamba hukumu zake zinachukuzana na maumbile na haja za mwanaadamu. Na miongoni mwa sura za wepesi katika hukumu za sheria ya Kiislamu, ni kwamba mtu anaye sumbuliwa na tatizo la kutokwa na mkojo (salasuli bauli); hana uwezo wa kuuzuia mkojo, swala yake inasihi kwa kufuata maelekezo yafuatayo:

  1. Asitie udhu ila tu pale anapotaka kuanza kuswali.
  2. Afunge utepe mahala unapotoka mkojo au akiweza avae kitambaa mfano wa nepi.
  3. Atwaharishe mahala unapotoka mkoja na atie udhu mpya kila anapotaka kuswali swala ya faradhi.

Ukunjufu wa mas-ala haya utaupata kwenye vitabu vya Fiq-hi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *