SWALI LA WIKI (JUMA LA 73)

SWALI:

Sheria inasemaje kuhusiana na mume aliye muingilia mke wake katika kipindi cha hedhi na je, hilo linamuwajibishia kutoa kafara. Na kama ndio, kafara yake ni nini?


JIBU: Jumuhuri ya Mafaqihi imepita ya kwamba kitendo cha mume kumuingilia mke wake akiwa katika hedhi, ni jambo lililo harimishwa na nukuu (nassi) ya kutinda iliyomo ndani ya Qur-ani. Ila tu ni kwamba kafara ya kitendo hicho cha haramu ni toba ya kweli na kuazimia kutokutenda tena mara nyingine.
Ama mtu kutoa sadaka kama kafara, zimepokewa kuhusiana na jambo hilo hadithi kadhaa na jambo hilo limechukuliwa juu ya usunna na si wajibu. Basi yeyote atakaye tenda tendo haramu hilo, kisha akatubia toba ya kweli na akataka kuongezea sadaka juu ya toba yake hiyo, sadaka itakayo waneemesha mafakiri. Basi kufanya hivyo kutakuwa ni kutenda kheri juu ya kheri na sadaka hiyo inaweza kutolewa na yeyote; mume au mke ingawa katika asili anaye takiwa kutoa ni mume, kwa sababu yeye ndiye aliye sababisha kutendeka kwa haramu.
Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *