SWALI LA WIKI (JUMA LA 72)

SWALI: Naomba kujua hukumu ya sharia kwa mwanamume ambaye hajafanya khitani (hajatahiriwa). Je, swala yake inajuzu?

JIBU: Khitani (tohara) ni katika jumla ya mambo ya kimaumbile yaliyo letwa na Uislamu na akayaamrisha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie. Nayo khitani ni faradhi isiyo epukika kwa wanamume na ni dharura (jambo la lazima) ya kiafya.

Ama matendo ya mtu ambaye hajakhitaniwa, ibada zake na miamala yake, hayo hayana mafungamano na kutahiriwa au kutokutahiriwa kwake kwa upande wa kusihi au kubatilika kwa matendo hayo ya kiibada na yale ya kimiamala.

Kubwa kabisa linalo patikana kwa mtu ambaye hakutenda mambo muhimu haya ya kimaumbile yaliyo letwa na Uislamu, ni kujitia kwenye hatari ya kupatwa na maradhi na pengine akawaambukiza na wengine. Na ni jambo lijulikanalo wazi ya kwamba mtu kupatwa na maradhi yoyote yale yawayo, hakukifanyi kichinjwa chake alicho kichinja kwa mkono wake, kuwa ni najisi; kisicho lika na wala hakufanyi ibada zake kuwa ni batili. Na wala hilo haliathiri chochote katika imani yake na kusalimika kwa dini yake. Na tena yeye atakapokufa, ataswaliwa, kukafiniwa na kuzikwa kwenye makaburi ya Waislamu.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *