SWALI LA WIKI (JUMA LA 71)

SWALI: Nina msahafu mkongwe ambao karatasi zake zimechanika chanika na haufai tena kutumika katika kusoma Qur-ani. Niufanyeje msahafu huo na je sharia inaniruhusu kuuchoma?

JIBU: Kwa kuwa msahafu haufai tena kusomea na kwa kuwa kurasa zake zimechanika chanika na kunahofiwa huenda zikapeperuka na kuangukia mahala pachafu au kukanyagwa na watu.

Basi lililo bora ni kuunguzwa moto ili kuhifadhi Qur-ani isidharaulike na kuvunjiwa heshima na ichomwe mahala palipo twahara na si majaani. Iunguzwe mpaka ichanganyike na mchanga na baadhi ya Mafaqihi wamesema kisha yachukuliwe majivu yake na kufukiwa shimoni.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *