SWALI LA WIKI (JUMA LA 62 )

SWALI: Je, sharia inaruhusu kutoa fungu katika mali ya marehemu kuwapa ndugu/jamaa zake mafakiri na wenye shida?

JIBU: Namna/njia ya kugawa zaka imeshabainishwa na Qur-ani Tukufu kupitia kauli yake Mola iliyomo ndani ya Surat-Taubah (09), aya ile ya 60, na tusome: “Hakika si vinginevyo, wa kupewa sadaka (zaka) ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika njia ya Allah, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Allah. Na Allah ni Mwenye kujua Mwenye hikima”.

Naam, iwapo marehemu anao ndugu zake mafakiri na wenye shida, kunajuzu kuwapa sehemu ya fungu la zaka kutoka kwenye mali ya marehemu ndugu yao na hilo ndilo lililo bora zaidi. Na wala si lazima kuyapa mafungu yote hayo manane yaliyo tajwa ndani ya aya, bali atatangulizwa kupewa yule mwenye shida zaidi kuliko wengine na ni bora kufuata utaratibu huu ulio elezwa na aya.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *