SWALI LA WIKI (JUMA LA 69)

SWALI: Nimeokota mtoto, nikampeleka nyumbani, mke wangu amefurahi na tumeamua kumlea na kumfanya mwanetu kwa kuwa sisi hatujajaliwa kupata mtoto. Nini hukumu ya kumuhalisi mtoto huyo (adoption)?

JIBU: Kumpa malezi, elimu na kumuandaa mtoto huyo kwa mustakabali mwema wa maisha yake, hilo ni jambo jema sana na lenye ujira adhimu mbele ya Mola. Lakini Uislamu hauruhusu kumuhalisi mtoto huyo, ukampa ubini wako kama mtoto wako wa kumzaa mwenyewe; wewe ukawa baba yake na mkeo akawa mama yake. Kwani kufanya hivyo ni kumtia katika familia yenu, jambo ambalo litampa haki ya kurithi ambayo haithibiti ila kwa kupitia nasabu. Na akirithi atakuwa amewazuia kupata mirathi wale wanao stahiki kisharia. Na pia jambo hilo linamjengea mazingira ya kuwarithi pia ndugu zenu nyie mke na mume. Jambo hilo halijuzu kisharia na Uislamu umekataza kumuhalisi mtoto muokotwa, lakini haujakataza kumlea, kwani hicho ni kitendo cha utu.

Tanbihi: Uislamu unaruhusu kumpa mtoto huyo chochote, mithili ya kumjengea nyumba au kumfungulia mradi utakao muingizia kipato katika kipindi cha uhai wa hao walezi wake, lakini si kupata mirathi baada ya kufariki kwao.

Allah ndiye Mjuzi mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *